MAMA KANUMBA:NAAPA NITAMFUNGA HUYU TAPELI.
MAMA KANUMBA
Baada ya hivi karibuni kuibuka tena kwa yule nabii na Mchungaji
George Kaiuruki na kudai kuwa Marehemue Steven Kanumba bado yu hai,
FROLA Mtegoa - mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji nyota filamu wa Bongo
marehemu Steven Kanumba amesikitishwa na tabia ya mtu anayejiita Nabii
George Kairuki kwa kutumia jina na kifo cha marehemu mwanaye kama njia
ya kujitengenezea fedha na umaarufu, mama Kanumba anasema kuwa awali
Kairuki alitumia msiba wa mwanaye katika kuongelea vitu ambavyo hata
familia haivijui isipo kuwa yeye pekee yake.
Mama Kanumba anadai kuwa hivi karibuni Kairuki alijitokeza kwa
kudai kuwa Kanumba hajafa na amemtumia fedha katika simu yake, na kusema
kuwa karibu atamrudisha duniani na kuendelea na maisha yake jambo
ambalo mama wa marehemu anapingana nalo kwa kusema kuwa yeye kwa imani
yake anaamini kuwa mwanaye amefariki na hakuna miujiza mingine.
“Huyu mtu anayeitwa Nabii George Kairuki sijui anatafuta nini
katika familia yangu, Kanumba alikuwa ni kipenzi cha watu na sisi sote
tumeshuhudia hilo kama kweli yeye ana uwezo wa kumfufua amfufue watu
wote watafurahi kipenzi chao kurudi kama anavyosema yeye, mimi simjui
hata sura zaidi ya kumuona katika picha,”anasema mama Kanumba
Mama Kanumba anasema kuwa iwapo Kairuki ataendelea na tabia hiyo
itabidi afanye utaratibu wa kumfungulia mashitaka na hata ikibidi
kumfungulia mashitaka na kumfunga endapo ataendelea na tabia ya kutumia
sana jina la Kanumba katika kujitafutia fedha na kutangaza maneno ya
ajabu ajabu.
Post a Comment