DOGO JANJA ATIMULIWA MTANASHATI ENTERTAINMENT
Abdulaziz Chende 'Dogo Janja'.
Msanii chipukizi wa muziki wa Hip Hop,
Abdulaziz Chende maarufu kwa jina la Dogo Janja, ametimuliwa katika
kundi la Mtanashati Entertainment.
Janja akiwa na PNC baada ya kuwasili jijini Dar tayari kujiunga na Mtanashati Juni 22, 2012.
Akizungumza na Mtandao huu, kiongozi wa Mtanashati Entertainment
Ustaadh Juma Namusoma alisema kuwa sababu za kumtimua Dogo Janja ni
utovu wa nidhamu, unywaji pombe, kutokwenda shule pamoja na uvutaji
bangi.
Aliongeza kuwa tayari amempatia nauli ya shilingi 90,000/= kurudi
nyumbani kwao jijini Arusha alipotokea. Dogo Janja alitua kwa mbwembwe
jijini Dar es Salaam kwa ndege Juni 22 mwaka jana akitokea Arusha na
kujiunga na kundi hilo.
Awali alikuwa katika kundi la Tip Top Connection linaloongozwa na
Madee lakini ilitokea kutoelewana kati yao na kurudishwa kwao Arusha.
Alipopigiwa simu na Mtandao huu, Dongo Janja alidai kuwa bado ni memba
hai wa Mtanashati Entertainment.
CHANZO CHA HABARI NI GLP
Post a Comment