BOSI NSSF ALIVYOCHINJWA KINYAMA
BOSI wa NSSF aliyeuawa kikatili kwa kuchinjwa eneo la Moshono jijini
Arusha, Regina Mushi amezikwa rasmi kijijini kwao Karansi, Kitongoji cha
Ashengai, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Jumamosi wiki iliyopita.
Regina Mushi enzi za uhai wake.
Akizungumza wakati wa mazishi hayo baba mzazi wa marehemu, Damas
Mushi alilaani tukio la kuuawa kikatili kwa binti yake huyo ambaye miaka
michache iliyopita alihitimu shahada yake katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na kuajiriwa katika Taasisi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)
ambapo alifanya kazi miaka miwili hadi kifo kilipomkumba Oktoba 14,
mwaka huu nyumbani alipokuwa akiishi Moshono, jijini Arusha.
Regina aliuawa kinyama chumbani kwake kwa kuchinjwa na kukatwakatwa
sehemu mbalimbali za mwili wake na hadi sasa haijafahamika sababu ya
kufanyiwa unyama huo.
“Siku chache kabla ya kifo cha mwanangu aliniambia kuwa ana mpango wa kuendelea kusoma kwa kiwango cha shahada ya pili lakini bahati mbaya ameuawa kikatili ni jambo la kusikitisha sana,” alisema mzazi huyo.

Ametoa wito kwa jeshi la polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa
kina wa tukio hilo ili kuwabaini na kuwatia mbaroni waliofanya unyama
huo.
Naye baba mdogo wa marehemu, Wakili Cornelius Kariwa amesema mauaji hayo ni kinyume cha sheria na ni kitendo cha kishetani.
Naye baba mdogo wa marehemu, Wakili Cornelius Kariwa amesema mauaji hayo ni kinyume cha sheria na ni kitendo cha kishetani.
“Ukatili wa namna hiyo wa kumchoma mtu visu ni wa hali ya juu kwani
ulisababisha kutapakaa na kujaa damu kitandani, ni ukatili uliopitiliza
ambapo hata angekuwa na kosa marehemu asingepaswa kupata adhabu ya aina
hiyo na kwamba kitendo hicho ni cha kulaaniwa katika jamii,” alisema
wakili huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo. “Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi
kuhusiana na tukio hilo,” alisema kamanda huyo.
CHANZO NI GLP

Post a Comment