KIFO TATA, KIONGOZI CCM AFIA KWA MGANGA.
Stori: Hamida Hassan na Gladness Mallya wa Global Publishers.
MJUMBE wa Serikali ya Mtaa wa Michungwani, Kimara King’ong’o jijini Dar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni kiongozi wa umoja wa wazazi, Seleman Hashim Ndege amefariki dunia nyumbani kwa mganga wa kienyeji ‘Sangoma’, Veronica Kasumen ‘mama
MJUMBE wa Serikali ya Mtaa wa Michungwani, Kimara King’ong’o jijini Dar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni kiongozi wa umoja wa wazazi, Seleman Hashim Ndege amefariki dunia nyumbani kwa mganga wa kienyeji ‘Sangoma’, Veronica Kasumen ‘mama
Misingo’ na kifo chake kuacha utata,
Ijumaa lina habari kamili.
Akizungumza kwa uchungu mke wa marehemu, Mwajuma Ally amesema kuwa
siku ya tukio (Jumamosi iliyopita) mume wake aliamka asubuhi saa 12 na
kwenda kusambaza vipeperushi vya kazi zake za serikali ya mtaa.
Mwajuma alisema ilipotimu saa tisa alasiri, alifuatwa na mama Misingo
na kumwambia kuwa mume wake amefariki dunia nyumbani kwake na kumtaka
waende kuuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka Hospitali ya Tumbi,
Kibaha.
“Nilishtuka sana kwa kuwa mume wangu hakuwa akiumwa chochote,
niliambatana na mama Misingo kwenda nyumbani kwake,” alisema Mwajuma
kwa unyonge.
Mke huyo aliendelea kudai kwamba alipotoka nje alikutana na gari la
Kituo cha Polisi cha Mbezi Kwa Yusuf waliomwamuru kuingia ndani ya gari
hilo aina ya Land Rover ‘Difenda’ huku wakimuuliza kama amemuona mume
wake.
“Kilichonishtua ndani ya gari kulikuwa na wanaume wengine
wawili wakanionesha mwili wa mume wangu ukiwa tayari umeshavalisha sanda
bila ya kunishirikisha,” aliendelea kusema Mwajuma...
Mke huyo
alisema kuwa alimhoji mama Misingo kilichotokea, naye akamwambia kuwa
mumewe alifika kwake kwa lengo la kumuona mtoto wake ambaye alianguka na
pikipiki lakini ghafla akaanguka na kuaga dunia mara baada ya kuomba
kuingia msalani.
“Tulienda mpaka Hospitali ya Tumbi ambapo mwili
ulihifadhiwa kisha tukarudi nyumbani,” alimaliza mke wa marehemu huku
akisema kuwa amebaki na utata juu ya kifo cha mumewe.
Naye Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Michungwani ambapo marehemu alikuwa akiishi, Fadhili Mzee Jakaya alisema alishtushwa na taarifa za kifo hicho na kuzifuatilia.
Naye Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Michungwani ambapo marehemu alikuwa akiishi, Fadhili Mzee Jakaya alisema alishtushwa na taarifa za kifo hicho na kuzifuatilia.
“Mimi na wenzangu tulienda Kituo cha Polisi cha Mbezi
lakini tulishangaa kukuta mganga huyo (mama Misingo) ameandikisha kuwa
ni mkazi wa Kibamba na aliyefariki ni kaka yake aliyefika nyumbani kwake
kumuona mpwa wake ndipo alipoanguka chooni, hicho kilitushangaza,”
alisema.
Jakaya alisema kitendo cha mganga huyo kudanganya eneo
analoishi na udugu wake na marehemu kiliwafanya waamini kuwa kulikuwa na
kitu nyuma ya pazia.
“Tunasikia Ndege alifariki saa tatu asubuhi,
imekuwaje wamekaa naye hadi saa tisa jioni, haya kama si maajabu ni
nini? Pia kwa nini wamvalishe sanda? Hapa kuna sababu zitajulikana tu,”
alisema Jakaya.
Wananchi wa Michungwani walijikusanya na kwenda
nyumbani kwa mama Misingo na kumkuta akiwa na mumewe ambapo walimhoji
kuhusu maelezo tata aliyoyatoa kituo cha polisi.
Hata hivyo, viongozi
wa serikali ya mtaa walitoa taarifa polisi ambao walifika nyumbani kwa
mganga huyo baada ya nusu saa na kuondoka naye.
Habari zilizopatikana
kutoka kwa majirani zinadai Ndege alifika nyumbani kwa mama Misingo na
kutibiwa kwa kupewa dawa lakini cha ajabu akafariki dunia.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa King’ongo anapoishi mama Misingo, Demetrius
Mapesi amesikitishwa na kitendo hicho na kusema iwapo vipimo vitabaini
kuwa dawa aliyokunywa marehemu ni sumu watachukua hatua kali.
Waandishi
wetu walifika nyumbani kwa mama Misingo na kuzungumza na watoto wake,
ambapo mmoja wao alisema kuwa, marehemu alifika nyumbani kwao saa tatu
asubuhi kwa lengo la kumuona kaka yao aitwaye George ambaye alikuwa
mgonjwa.
“Baada ya muda aliomba kwenda chooni na kukaa huko kwa muda
mrefu, mama akamsikia akikoroma ndipo akaniambia nivunje mlango nimtoe.
“Nilifanya
hivyo, tulikuwa na mama na mzee mmoja (jina linahifadhiwa) tulijaribu
kumvua nguo na kumwagia maji lakini alikuwa tayari ameshafariki dunia,
mama akapiga simu kuwaita polisi,” alisema mtoto huyo.
Naye jirani
mwingine wa mama Misingo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema
hawakupewa taarifa za mtu kuanguka chooni na alipoliona gari la polisi
limewabeba alihoji na kuambiwa kuwa hakukuwa na tatizo lolote.
Baada
ya kufanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Tumbi, mwili wa marehemu
uliagwa nyumbani kwake Kimara Michungwani kisha kusafirishwa kwenda
Mtwara kwa ajili ya mazishi ambapo mtaani vilio vilitawala kila kona
wakati wa kuuaga mwili.
Bado wakazi wa Kimara Michungwani wanasubiri taarifa ya daktari ili kujua kilichosababisha kifo cha Ndege.
CHANZO NI Global Publishers.

Post a Comment