HATIMAYE LEWANDOWSKI KUSAINI BAYERN MUNICH MWEZI JANUARY - MWENYEWE ATHIBITISHA.
Mshambuliaji
wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski amethibitisha rasmi kwamba
atasaini mkataba wa kwanza wa makubaliano wa kujiunga na Bayern Munich
katika soko la usajili la mwezi wa January kisha kujiunga na mabavaria
mara tu mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.


Baada
ya tetesi za muda mrefu kuhusu mshambuliaji huyu wa kipoland, hatimaye
hivi sasa ipo wazi Pep Guardiola atamuongeza mshambuliaji katika kikosi
chake 2014.
Kwa mara ya kwanza mchezaji amekiri kwamba atajiunga na Bayern mwishoni mwa msimu wakati alipokuwa akihojiwa na Sport 1, alisema: ‘Ndio, nathibithisha nitahamia Bayern kwa sababu sasa hivi nikasaini mkataba wa makubaliano.
Post a Comment