ad

ad

UVCCM Arusha wazidi kushambuliana.

Arusha. 
Sakata la Kaimu Katibu wa UVCCM Arusha, Masoud Rajabu kukamatwa na kisha kupewa kipigo na viongozi wenzake ndani ya umoja huo, limechukua sura mpya baada viongozi wa umoja huo kushambuliana vikali kwa kutoleana lugha za matusi


Masoud alishambuliwa kwa kupigwa na viongozi wenzake hivi karibuni mara baada ya kutuhumiwa kukusanya fedha za miradi mbalimbali bila idhini ya uongozi wa jumuiya hiyo, ambapo mbali na kupigwa pia aliporwa kiasi cha Sh140,000 na viongozi hao.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mara baada ya tukio hilo Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, Robinson Meitinyiku aliamua kuitisha kikao cha pamoja juzi kujadili tukio hilo.

Habari zilidai kuwa mara baada ya wajumbe kuwasili kikaoni, ndipo mwenyekiti wa umoja huo mkoani hapa aliwasomea ajenda za kikao lakini wakati wa kuchangia ndipo hali ya hewa ilianza kuchafuka.
Powered by Blogger.