TAIFA STARS YAPANGWA NA NAMIBIA, MAURITIUS NA SWAZILAND KATIKA MICHUANO YA COSAFA.
TIMU ya taifa ya Tanzania,
Taifa Stars inatarajiwa kukutana na timu ngumu ilizopangiwa katika kundi A
kwenye ratiba ya michuano ya inazozishirikisha nchi zilizopo kusini mwa
Afrika-COSAFA iliyopangwa jana jijini Lusaka, Zambia.
Katika kundi A Taifa Stars
imepangwa kuchuana na timu za Namibia, Mauritius na Swaziland ambapo mshindi
katika kundi hilo atakutana na Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali.
Stars itakwaana na Swaziland Julai jijini Lusaka kabla ya kukutana na Mauritius
Julai 8 hapohapo Lusaka huku mchezo wa mwisho dhidi ya Namibia ukitarajiwa
kuchezwa Julai 10 jijini Kabwe.
Stars ambao kwa kipindi cha hivi karibuni
wameonyesha kuwa na kiwango cha kutisha wanategemea kushinda michezo yao na
kuibuka mshindi kwenye kundi hilo na kutinga hatua ya robo fainali kucheza na
Bafana Bafana ambao ni mabingwa mara tatu wa michuano hiyo.
Post a Comment