MSEMAJI
MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA JOSEPH O. MBILINYI (MB) KUHUSU
MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI
NA MICHEZO KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014
(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99 (9) ya kanuni za Bunge toleo la mwaka 2013) 1. UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika,
Dira ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni “kuwa na
taifa lililohabarishwa vizuri, lina vijana wenye uwezo na malezi bora,
linathamini utamaduni wake na linakuwa mahiri katika michezo ifikapo
mwaka 2025.” Aidha, ‘dhamira’ ya wizara hii ni ‘kuendeleza utambulisho
wa taifa kwa kuwezesha upatikanaji mzuri wa habari, kuwawezesha vijana
kiuchumi na kukuza utamaduni na michezo kwa umma kwa maendeleo ya
kijamii na kiuchumi.’
Mheshimiwa Spika, Kwa maoni ya Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni, Serikali hii ya CCM imeshindwa kutekeleza
dira na dhamira iliyotajwa katika maandiko ya kisera ya Wizara. Badala
yake, chini ya usimamizi wa Wizara hii, Tanzania imegeuka kuwa taifa
lisilotaka watu kuhabarishwa vizuri juu ya matendo ya watawala.
Tanzania
imegeuka kuwa taifa linalofungia magazeti yanayofichua ufisadi, uchafu
na matumizi mabaya ya madaraka miongoni mwa viongozi, watendaji na
watumishi wa Serikali hii ya CCM. Tanzania imegeuka, chini ya usimamizi
wa Wizara na Serikali hii ya CCM, kuwa taifa linaloteka nyara
wanahabari, kuwatesa kwa kuwang’oa kucha na meno, kuwatoboa macho,
kuwamwagia tindikali na hata kuwaua. Tanzania sio nchi inayoandaa vijana
wake tena.
Haiwapi tena elimu bora wala kuwapatia maarifa, uwezo na
malezi bora; ni nchi isiyowawezesha wala kuwathamini vijana wake; ni
nchi inayoruhusu vijana wake kunyonywa na kutoendelezwa; na ni taifa
ambalo limeachia utamaduni utambulisho wake kama taifa kupotea kabisa.
Aidha, katika fani ya michezo ya aina zote, Tanzania imeporomoka kutoka
taifa lililokuwa linaheshimika kimataifa katika miaka ya sabini na kuwa
alichokiita rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ‘kichwa cha mwendawazimu’
ambacho kila kinyozi anajifunzia kunyolea!...
Post a Comment