Malkia wa Nyuki aipeleka Simba SC England.
MLEZI wa Simba, Rahma Al Kharusi amevunja ukimya wa muda mrefu na kusema
anaendelea kufanya shughuli za klabu hiyo kwa kuwa sasa yuko nchini
England.
Rahma maarufu kama Malkia wa Nyuki amesema yuko jijini
London kwa ajili ya mkutano maalum na mmiliki wa Sunderland, Ellis
Short, kujadili mambo kadhaa kwa faida ya klabu hizo na hasa Simba.
“Nipo,
kama nilivyosema awali, zaidi nimewekeza nguvu zangu kwa ajili ya msimu
ujao. Sasa niko London na baadaye nitaenda Sunderland kwa ajili ya
kukutana na mmiliki wake.
“Kuna masuala kadhaa ya msingi kuhusiana na uhusiano mpya wa Simba na Sunderland, najua Simba ndiyo itafaidika zaidi.
“Ratiba
ni kwamba nitakutana na watu wa Sunderland na ratiba yao na mimi
itakuwa kuanzia Jumapili hadi Jumanne,” alisema Malkia wa Nyuki.
Taarifa zinaeleza huenda Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, naye akaungana na Malkia wa Nyuki nchini humo leo na kesho.
Taarifa zinaeleza huenda Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, naye akaungana na Malkia wa Nyuki nchini humo leo na kesho.
Akiwa
jijini Dar, mwezi uliopita, Malkia wa Nyuki alizungumza na Short
kuhusiana na suala la uhusiano wa klabu hizo mbili na mmiliki huyo
bilionea wa Sunderland akatoa mwaliko huo.
Iwapo Simba itafanikiwa kuingia mikataba ya kimaendeleo na Sunderland yenyewe ndiyo itafaidika zaidi kwa kuwa Waingereza hao wamepiga hatua zaidi kimaendeleo.
Iwapo Simba itafanikiwa kuingia mikataba ya kimaendeleo na Sunderland yenyewe ndiyo itafaidika zaidi kwa kuwa Waingereza hao wamepiga hatua zaidi kimaendeleo.
Post a Comment