UKIWACHUKIA BARCELONA, MESSI LAZIMA UKONDE, AC MILAN YATUPWA NJE CHAMPIONS LEAGUE …HISTORIA MPYA YAANDIKWA
DAKIKA
ya 5 Lionel Messi anaifungia Barcelona bao kwanza, AC Milan
wanachukulia poa na kujiona bado wako mchezoni, dakika ya 40 Messi tena
linakuwa bao la pili, timu zinakwenda mapumziko 2-0.
Kipindi
cha pili kinaanza, Barcelona wanagonga pasi za ajabu, Messi anafanya
atakavyo, dakika ya 55 anatoa pasi iliyosababisha goli lililofungwa na
David Villa, AC Milan wanacharuka lakini wanakuwa wamechelewa, wanapigwa
bao la nne katika dakika ya mwisho ya mchezo kupitia kwa beki wa
kushoto Jordi Alba.
Hivyo
ndivyo ilivyokuwa katika dimba la Nou Camp palipochezwa mchezo mkali wa
marudiano wa ligi ya Mabingwa Ulaya na kutoa matokeo yaliyowaduwaza
wengi.
Ukichanganya magoli 2-0 ya AC Milan katika mchezo wa kwanza uliofanyika San siro, Barcelona wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 4-2.
Barcelona
wanaandika historia na kuwa timu ya kwanza katika michuano ya klabu
bingwa Ulaya kuingia uwanjani wakiwa nyuma 2-0 na kasha kusonga mbele.
Hakuna timu iliyowahi kufanya hivyo.
Barcelona
walihesabiwa kama wameshatolewa wiki mbili zilizopita, lakini juzi
Messi alitoa tahadhari kuwa kwa wale wote wanaodhani kuwa
wamesambaratika basi wajue wanajidanganya.
Chanzo saluti 5-Tanzania
Post a Comment