Moshi mweusi Vatican, Bado hakuna Papa
Moshi mweusi umetokea kwenye dari la hekalu ya
Sistine mjini Roma, kumaanisha kuwa makadinali walioko ndani ya hekalu
wameshindwa kuafikiana juu ya Papa mpya anayetarajiwa kuchaguliwa.
Moshi mweupe utaashiria kupatikana kiongozi mpya wa kanisa Katoliki la Roma.
Makadinali
hao wanatarajiwa kupiga kura mara nne kwa siku hadi pale thuluthi mbili
ya makadinali wote watakapoafikiana juu ya Papa mpya.
Walipiga kura yao ya kwanza ambayo haikuleta
maafikiano hapo usiku wa Jumanne. Yeyote atakayeteuliwa kuliongoza
kanisa hilo katoliki anakabiliwa na wakati mgumu, ambapo kanisa
limezongwa na kashfa mbali mbali pamoja na migawanyiko ya ndani.
Papa aliyeondoka Benedikt wa Kumi na sita
aliwashangaza wengi alipotangaza kujiuzulu wadhifa huo miaka minane tu
tangu kuchaguliwa. Yeye ndiye Papa wa kwanza kujiuzulu katika miaka 600
ya historia ya kanisa hilo.
Alitoa sababu kuwa amezeeka na afya yake
imedhoofika kwa hivyo haoni kuwa anaweza kutekeleza wajibu wake
kikamilifu kama Papa wa kanisa.

Post a Comment