Wanafunzi
waliofukuzwa vyuo vikuu nchini wamemuomba Rais Jakaya Kikwete kuingilia
kati tatizo lao ili kuwawezesha kuhitimu masomo katika fani mbalimbali.
Wanafunzi hao chini ya muungano wao wanaouita Umoja wa Wanafunzi
waliofukuzwa Vyuoni wanasema kurejea katika masomo na kuhitimu
kutaongeza idadi ya wataalamu katiki sekta za uzalishaji nchini.
Wanasema awali walibisha hodi ofisi za Bunge kusaka muafaka wa tatizo
lao bila mafanikio huku safari hii wakimuomba Rais kuingilia kati…
Umoja huo wa wanafunzi unahusisha wanafunzi kutoka Chuo Kikuu Dodoma,
Chuo Kikuu Cha Muhimbili, Mwalimu Nyerere na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha
IFM.
Wanafunzi hao zaidi ya 50 ni miongoni mwa walifukuzwa
Chuo mwaka 2011 baada ya kugoma kwa lengo la kuishinikiza serikali
kuwaongezea fedha za kujikimu.
Post a Comment