Kim Kardashian aelezea hali anayokutana nayo baada ya kubeba mtoto wa Kanye West tumboni, “bado sio kitu rahisi..”
![]() |
| Kanye West & Kim Kardashian |
Habari za mrembo Kim Kardashian kuwa na ujauzito zili-make
headline sana kwenye mitandao mbalimbali, ikiwa ni ujauzito wa kwanza kwa
mrembo huyo ambao ameupata kwa boyfriend Kanye West ambae amekuwa akielezea
hisia zake za ndani kwa mrembo huyo publically na hata kwenye mistari yake ya
nyimbo.
K.K mwenye ujauzito wa miezi mitatu amefunguka kuhusu
mabadiliko ya mwili wake baada ya kumbeba mtoto wa wa Kanye West tumboni kwa
miezi mitatu hivi sasa. Mwanamitindo kutoka the Kardashian amesema bado
hajajisikia kuwa na homa za asubuhi hadi sasa, dalili ambazo wanawake
wajawazito hukutana nazo, na kwamba bado anajizoeza hali mpya ya mwili wake.
“nimejisikia vizuri. Sijaugua homa za asubuhi hadi sasa,
lakini bado sio kitu rahisi sana,” alifunguka Kim K alipokuwa amhudhuria party
ya kufunga mwaka huko Las Angeles katika 10AK night club, usiku wa mwaka mpya.
Ameonekana kuenjoy hali yake ya ujauzito wa kwanza kwa
kipindi hiki cha miezi mitatu, na amesema huwa anasikia watu wanasema ni rahisi
and it’s fun, lakini yeye anasema sio rahisi sana, “It’s definitely an
adjustment leaning about your body and stuff like that,” alifunguka Kim
Kardashian na kukazia, ‘nimekuwa najisikia vizuri, vizuri kweli.”

Post a Comment