ad

ad

HAKUNA KAMA MESSI …ATWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA DUNIA KWA MARA YA 4 MFULULIZO


LIONEL Messi ameweka rekodi mpya ya kuwa mtu wa kwanza katika historia ya soka kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia ‘Ballon d'Or’ kwa mwaka wa nne mfululizo.
FINE MESS ... Messi receives the 2012 Ballon D'Or from Fabio Cannavar
Messi akipokea tuzo yake ya nne mfululizo
Messi mwenye umri wa miaka 25 ametwaa tuzo hiyo iliyokuwa pia inawaniwa na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Andres Iniesta wa Barcelona.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Messi ambaye hivi karibuni alivunja rekodi ya miaka 40 ya Gerd Muller kwa kufunga magoli 91 ndani ya mwaka mmoja, anafanikwa kuwaacha nyuma nyota wa zamani wa Uholanzi Johan Cruyff na Marco Van Basten  pamoja na mfaransa Michel Platini (Rais wa sasa wa UEFA) walioshinda tuzo ya Ballon d'Or mara tatu.
Lionel Messi wins Ballon D'Or
Ronaldo, Iniesta, Messi wakiwa katika picha ya pamoja
“Kusema kweli, kushinda tuzo hii mara nne ni jambo la kustaajabisha, ni heshima kubwa ambayo siwezi kuizungumzia” alisema Messi
“Napenda kutoa shukrani zangu kwa wachezaji wenzangu wa Barcelona, Andres Iniesta imekuwa ni faida sana kucheza na kufanya mazoezi pamoja nawe, nakushukuru sana.
“Pia nawashukuru wenzangu katika timu ya taifa ya Argentina, kuanzia wachezaji, makocha na wote niliofanya nao kazi” alisema Messi.
Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente Del Bosque alishinda tuzo ya kocha bora na kuwashinda Pep Guardiola na Jose Mourinho wa Real Madrid ambaye hakuhudhuria sherehe hizo.
THREE AND EASY ... Lionel Messi has won the past three Ballon d'Or awards
Messi katika tuzo zake tatu zilizopita
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo alisema kama atashinda itakuwa poa, akishindwa hakuna noma, maisha yanaendelea.
“Hata hivyo lazima nikiri kuwa ningependa kushinda tuzo hii, nisiwe mnafiki juu ya hilo” alisema Nyota huyo wa zamani wa Manchester United muda mfupi kabla ya tuzo hizo kutolewa.
“Iwe kihalali au kinyume chake, matokeo yataendelea kusimama kama yalivyo, naweza nikawa mtu wa furaha au huzuni, hayo ndio maisha” aliongeza.
WHAT A LINE UP ... the FIFA/FIFPro World XI, top (l-r): Ronaldo, Marcello, Ramos, Pique, Alves, Casillas. Bottom (l-r) Falcao, Messi, Iniesta, Xavi, Alonso
Kikosi cha wachezaji 11 bora wa dunia
Katika sherehe hizo zilizofanyika nchini Uswisi, kilitajwa kikosi  cha wachezaji 11 bora wa dunia ambako hakuna hata mchezaji mmoja aliyetoka nje ya ligi kuu ya Hispania.
Kikosi hicho ni: Casillas (Real Madrid), Alves (Barcelona), Pique (Barcelona), Ramos (Real Madrid), Marcelo (Real Madrid), Xavi (Barcelona), Alonso (Real Madrid), Iniesta (Barcelona), Messi (Barcelona), Ronaldo (Real Madrid), Falcao (Atletico Madrid).
Powered by Blogger.