WAAMUZI
18 na washika vibendera 21 wameteuliwa kuchezesha mechi za michuano ya
Mataifa ya Afrika-Afcon itakayoanza kutimua vumbi Januari 19 mwaka huu
nchini Afrika Kusini. Kuna
mabadiliko mawili kwa upande wa waamuzi na nane kwa upande wa washika
vibendera kulinganisha na wale ambao walichezesha fainali za michuano
hiyo zilizofanyika nchini Equatorial Guinea na Gabon mwaka jana. Katika
orodha hiyo inajumuisha waamuzi wawili ambao wamechezesha fainali
zilizopita akiwemo Komlan Coulibaly kutoka Mali aliechezesha fainali ya
mwaka 2010 nchini Angola na Badar Diatta wa Senegal alichezesha fainali
ya mwaka jana kati ya Zambia na Ivory Coast jijini Libreville. Coulibaly
mwenye umri wa miaka 42 anatarajia kuweka rekodi ya kuwa mwamuzi
alichezesha Afcon mara nyingi zaidi ambapo hii ikiwa ni mara yake ya
saba toka alipoteuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2002. Waamuzi wawili
ambao wameteuliwa kwa mara ya kwanza ni pamoja na Sylvester Kirwa kutoka
Kenya na Bernard Camille kutoka Seychelles.
Post a Comment