ad

ad

Yanga Yazindua Jezi Mpya za Msimu wa 2026/27, Wanayanga Wavamia Jangwani

 

 

Klabu ya Young Africans SC (Yanga) imezindua rasmi jezi zake mpya zitakazotumika katika msimu wa mashindano wa 2026/27, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa soka.

Jezi hizo mpya zenye miundo mitatu tofauti kwa ajili ya mechi za nyumbani, ugenini na jezi mbadala, zimeendelea kubeba rangi na utambulisho wa klabu hiyo kupitia mchanganyiko wa kijani, njano na nyeusi.

Baada ya kutambulishwa rasmi, jezi hizo zimepokelewa kwa hamasa kubwa na mashabiki wa Yanga ambao wamejitokeza kwa wingi katika Makao Makuu ya klabu hiyo, Jangwani jijini Dar es Salaam, wakitaka kupata nakala zao mpya.

No comments

Powered by Blogger.