ad

ad

Scholes Aishauri Man United Kumsajili Cristian Romero Kutoka Tottenham

 


Nguli wa Manchester United Paul Scholes ameishauri klabu yake ya zamani kufanya usajili wa beki wa Tottenham Hotspur, Cristian Romero, akidai kuwa mchezaji huyo hafurahii maisha ya Spurs na anaweza kuwa chaguo sahihi kwa Old Trafford.

Scholes amesema anamkubali sana Romero na anaamini tabia yake ya kupambana uwanjani inaweza kuipa United uimara mkubwa safu ya ulinzi.

Beki huyo wa Argentina, ambaye ni bingwa wa Kombe la Dunia 2022, alikuwa uwanjani mwishoni mwa wiki wakati United ilipoichapa Spurs mabao 2-0, lakini alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Casemiro.

Tukio hilo limezua mjadala mkubwa, huku baadhi ya wachambuzi wakimuita “liability” kutokana na makosa yake ya mara kwa mara.

Tangu ajiunge na Tottenham mwaka 2021 kwa ada ya pauni milioni 47, Romero tayari amepewa kadi nyekundu nne katika Ligi Kuu England, idadi kubwa zaidi kwa mchezaji yeyote katika kipindi hicho.

Mbali na hilo, nahodha huyo wa Spurs amekuwa akikosolewa pia kwa kuikosoa bodi ya klabu kupitia mitandao ya kijamii, akilalamikia hali mbaya ya kikosi chao hasa kipindi walichobaki na wachezaji wachache waliokuwa fiti kutokana na majeraha mengi. Katika moja ya posti zake, aliita hali hiyo kuwa “ya aibu.”

Hata hivyo, Scholes anaamini hali hiyo inaonyesha tu kwamba Romero tayari ameichoka Spurs na anahitaji changamoto mpya.

Akizungumza kwenye podcast ya The Good, The Bad and The Football, Scholes alisema:

“Namkubali sana. Napenda kumtazama akicheza.
Anaonekana kama amechoshwa na Spurs, kama hataki kuwa pale tena.”

Kwa maoni ya Scholes, Romero ni “character” mwenye moyo wa kupambana, kitu ambacho anaamini kinaendana na utamaduni wa Manchester United.

No comments

Powered by Blogger.