ad

ad

Zari Athibitisha Wema Kuvunja Mahusiano Yake Na Diamond (Video)

Mfanyabiashara na mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zarinah Hassan 'Zari The Boss Lady'.
  Mfanyabiashara na mpenzi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zarinah Hassan 'Zari The Boss Lady' amesema kurudiana na Diamond haiwezekani na ataendelea kuwa Boss Lady kuimarisha zaidi biashara zake sababu alikuwa hivyo hata kabla ya kukutana naye. Akizungumza na Kituo cha BBC nchini Uingereza alikoenda kikazi, Zari alisema anaendelea na maisha yake ya kuandaa matamasha pamoja ku-host na anatarajia kuja na 'realty show' yake inayokwenda kwa jina la Life of Zari The Boss Lady. “I do a lot of things, kwanza ujue even before nimemkuta Diamond, nimekuwa nafanya appearances, nimekuwa Zari The Boss Lady even before Diamond, so I continue nitakuwa nafanya appearances, nitakuwa nafanya show, so I continue do the same thing,” anasema Zari. Katika hatua nyingine Zari amefunguka iwapo kinachoendelea ni kiki au kina ukweli wowote, Zari amesema kinachoendelea ni ukweli mtupu na kabla ya kutangaza uamuzi wake wa kumuacha Diamond walikaa wiki tatu bila kuzungumza. “Yaani tumeachana kabisa it’s done, tangu zile video zimetoka na ex wake (Wema Sepetu) nikawa nimempiga block at a time, tukawa hatujaongea three week after that ndio nikaposti, nimeamua nijiweke kando kabisa, I don’t need to be emotional, so I don’t real to speak more about this issue,” ameeleza. Alipoulizwa iwapo Diamond ameshamuomba msamaha au yupo tayari kumsamehe, alijibu; “Ameshakuja kipindi fulani, kipindi amezaa na yule dada fulani (Hamisa Mobetto), so sasa hivi sidhani kama inawekezana tena."

No comments

Powered by Blogger.