Shahidi: Wema Sepetu Alinambia anavuta Bangi kwa starehe
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imeendelea na kesi inayomkabili muigizaji Wema
Sepetu ambapo Ofisa wa Polisi WP Mary ameieleza mahakama kuwa mnamo
Februari 4, 2017 Wema alimwambia anatumia bangi kwa ajili ya starehe na
si kuuza
WP
Marry ambaye ni shahidi wa tatu ameyaeleza hayo wakati akiongozwa na
Wakili wa serikali Costantine Kakula, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas
Simba.
WP Marry amedai kuwa Wema alimueleza maneno hayo wakati walipokuwa njiani kuelekea nyumbani kwake kumkagua.
Amedai
kuwa February 4, 2017 aliagizwa kumtoa Wema Mahabusu na kwenda
kumfanyia upekuzi nyumbani kwake akiwa na OC CID na Maofisa wengine wa
Polisi.
Amedai
kuwa wakiwa wanajiandaa kuondoka Central Polisi kuelekea kwa Wema Bunju
Basihaya, wakiwa kwenye gari kuelekea huko alimuuliza Wema kuhusu
tuhuma zinazomkabili kwamba anahusika na biashara ya Dawa za kulevya au
kutumia.
Amedai kuwa Wema alijibu “Sijishughulishi na kuuza ila natumia bangi kama starehe”.
WP
Marry amedai kuwa baada ya kumuuliza Wema alimwambia mara yake ya
mwisho kuvuta Bangi ilikuwa Jumatatu ambapo swali hilo aliulizwa
February 4,2017.
Alieleza
kuwa walipofika nyumbani kwa Wema waligonga geti na kufunguliwa na
mdada wa kazi ambapo walivyoingia ndani walikuta kuna mdada mwingine wa
kazi.
WP
Marry amedai kuwa kabla ya kuingia ndani Wema aliomba kumpigia simu
dada yake ili awepo wakati wa kufanya ukaguzi ambapo dada yake alifika
na kujitambulisha kwa jina la Nuru Sepetu.
WP
Marry ameeleza kuwa wakati Wema anampigia simu dada yake alitoka dada
mmoja wa kazi kumfuata mjumbe ambapo alikuja naye na kujitambulisha kwa
jina la Steven Ndaho.
Amedai
baada ya dada yake Wema kufika alitaka kuwapekua kabla ya kuingia ndani
ambapo Nuru aliwapekuwa wote kabla ya kuingia ndani.
Amedai
baada ya kumaliza upekuzi walirudi Central polis, February 8,2017 saa
nne asubuhi alipewa maelekezo na Inspekta Wille kwamba aende na Wema kwa
Mkemia Mkuu wa serikali kwa ajili ya kuchukuliwa sampuli ya mkojo.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi March 12 na 13, 2018 kwaajili ya kuendelea na ushahidi.
Post a Comment