Lipumba kufukuza Madiwani Wote wa CUF Dar es Salaam
Naibu
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF kwa upande wa
Maalim Seif, Mbarala Maharagande amefunguka na kuweka wazi kuwa Profesa
Lipumba pamoja na genge lake wamepanga njama kuwafukuza madiwani wote wa
CUF Dar es Salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari Mbarala Maharagande amesema kuwa Lipumba
amepanga njama za kuwafukuza madiwani wa CUF Dar es Salaam wakiwepo
wastahiki Meya kutokana na madiwani hao kutokuwa na ushirikiano na
Lipumba na kundi lake.
"Lipumba
amepanga njama za kutaka kuwafukuza uanachama madiwani kwa tiketi ya
CUF-Chama cha Wananchi mkoa wa Dar es salaam; wakiwemo wastahiki Manaibu
Meya, kutokana na madiwani hao kukataa kumsaidia msaliti Lipumba na
genge lake katika kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kinondoni.
" Lipumba na watu wake wamejikuta katika wakati mgumu kwa uamuzi wao wa kusimamisha mgombea wakipingana na uamuzi wa UKAWA wa kusimamisha mgombea mmoja kutoka miongoni mwa vyama washirika.
"Uamuzi huo wa Lipumba ambao umetafsiriwa kuwa ni mpango wa kutaka kuzigawa kura ili kuisadia CCM ishinde, umeshitukiwa na wananchi wa jimbo la Kinondoni na kusababisha kususiwa mikutano yao ya kampeni na wadau mbalimbali"

Mbali
na hilo Maharagande amedai kuwa chama hicho kimejipanga vyema
kukabiliana na njama hizo zinazotaka kufanywa na Profesa Ibrahim Lipumba
"Tayari jopo la wanasheria wa Chama (CUF TAASISI) wamejipanga kukabiliana na hujuma hiyo vilivyo.
"Tutaendelea kutoa taarifa kwa wanachama wote na umma wa Watanzania kwa ujumla juu ya kila kinachoendelea kwa wakati muafaka.
"Tunatoa wito kwa wanachama wote, wapenda mabadiliko na demokrasia kwa ujumla kuzidi kuwa wastahimilivu na kuongeza kasi ya ushiriki wa shughuli mbalimbali za CUF Taasisi katika hatua hizi za mwisho za kumalizana na Wasaliti wa Mabadiliko na Demokrasia nchini" alisisitiza

Post a Comment