Breaking News: CCM Yaibuka Kidedea Ubunge Kinondoni (Video)

TUME ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Maulid Mtulia wa Chama cha Mapinduzi(CCM) kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa Ubunge, Jimbo la Kinondoni baada ya kupata kura 30,313 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Salum Mwalim (CHADEMA) aliyepata kura 12,353 na Rajab Salum wa CUF aliyepata kura 1,943. “Kwa matokeo hayo na kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa na sheria ya uchaguzi, namtangaza Maulid Mtulia kuwa Mbunge wa Kinondoni,” amesema msimamizi huyo wa uchaguzi. Jana jioni Februari 17,2018 Kagurumjuli alisema kazi ya kutangaza matokeo ingekamilika saa sita usiku lakini hilo lilishindikana.

Post a Comment