ad

ad

MAKOSA YALIYOMFU- KUZISHA ZITTO CHADEMA

Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe.
Stori: Mwandishi Wetu
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ambaye ametangazwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa amefukuzwa uanachama aliponzwa na mambo kadhaa.


Mawakili wa Chadema, Peter Kibatala, Tundu Lissu na John Mallya wameainisha kuwa  kesi hiyo kufunguliwa Mahakama Kuu haikuwa sahihi kwa kuwa ilipaswa kufunguliwa katika Mahakama ya Wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa mujibu wa kesi za madai.
Wanasheria hao walisema kesi hiyo ilikosewa pia kufunguliwa katika Masijala ya Mahakama Kuu badala ya kufunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Lissu alisema juzi kwamba Zitto alikuwa naibu katibu mkuu hivyo anaijua katiba yao ambayo inakataza mwanachama kupeleka mahakamani mambo ya chama na badala yake anatakiwa kufuata vikao husika ndani ya chama, hivyo kupeleka shauri hilo kortini maana yake ni kwamba amejivua uanachama kwa mujibu wa katiba yao.

“Kilichobaki sasa tunamwandikia barua mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kutimiza taratibu tu kwamba huyu Zitto si mwanachama wa Chadema,” alisema Lissu.
Zitto alipotafutwa alisema kwa sasa anaendelea na majukumu yake ya kazi kama kawaida.
 

“Kwa sasa naendelea na shughuli zangu kama kawaida ila ninashauriana na mwanasheria wangu cha kufanya. Nitaeleza nini cha kufanya baada ya kupata taarifa rasmi,” alisema Zitto.

Itakumbukwa kuwa Kamati Kuu ya Chadema iliwavua uanachama na nyadhifa zao Samson Mwigamba aliyekuwa kiongozi wa Mkoa wa Arusha na Profesa Kitila Mkumbo kutokana na madai ya kuandaa waraka wa mkakati wa mabadiliko ambao ulilenga kukiangamiza chama hicho.

Katika waraka huo, inadaiwa Zitto anatambuliwa kama MM (Mhusika Mkuu, Profesa Kitila M1 (Mhusika wa kwanza), na Mwigamba M3 (Mhusika wa tatu).Kesi ya Zitto aliyoiomba mahakama zuio la muda asivuliwe uanachama ilivuta hisia za watu wengi na kuwafanya wanachama wa Chadema kugawanyika makundi mawili ambapo kila ilipokuwa ikitajwa, walikuwa wakijazana mahakamani huku wengine wakimzomea na wengine wakimkingia kifua.
Zitto alijiunga na Chadema Aprili mwaka1993 na licha ya ubunge, alishika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama hadi akafikia ngazi ya unaibu katibu mkuu (Bara).

No comments

Powered by Blogger.