Michirizi Ya Damu - 09
“Who are you?” (wewe nani?) aliuliza Keith kwani kwa jinsi Fareed alivyoingia ndani ya chumba kile, alionekana kama mtu mwenye haraka nyingi.
“Nobody!” (si mtu yeyote) alijibu Fareed,
Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake aliyokuwa akiisubiri kwa hamu. Akamsogelea Keith mahali pale, alipomfikia, akamziba mdomo, hakutaka kuchelewa, akamchoma kisu mara tatu tumboni kisha kumlaza chini.
Hakukuwa na mtu aliyeona tukio hilo, kulikuwa na mwanga hafifu na kila mtu alikuwa na mpenzi wake katika vyumba vingine. Fareed alipohakikisha mwanaume huyo amekufa, akatoka ndani ya chumba kile na kuelekea katika chumba alichokuwemo.
“Ulikwenda wapi?” aliuliza Maria huku akimwangalia Fareed.
“Kwani hukuniona?”
“Hapana! Ulijificha?”
“Ndiyo! Nilidhani unakuja na bwana wako!” alisema Fareed.
Akamkumbatia Maria na hapohapo kubadilishana mate. Mwili wa Maria ukasisimka mno, hakuamini kama kweli siku hiyo alikuwa na mwanaume huyo.
Hakutaka kurudi kwa Keith, alikuwa tayari kugombana naye lakini si kumuacha mwanaume huyo ambaye kwake alikuwa mwanaume mzuri, hakuwa radhi kumuacha.
Wakaendelea kuangalia mambo ya historia mpaka walipoitwa ambapo walitakiwa kukusanyika na kuondoka. Maria aliogopa, alijua fika kwamba Keith angemuona na kumkaripia kwa kile alichokuwa amekifanya.
Akakiinamisha kichwa chake, akashangaa mpaka wanatoka, hakumuona mwanaume huyo na wala hakusikia kuitwa. Walipofika nje, haraka sana Fareed akamwambia waondoke kitu ambacho kwa Maria hakukuwa na tatizo.
“Na bwana wako akikuulizia?” alimuuliza.
“Nitamwambia niliondoka na shangazi. Ila subiri, mimi ni mtoto wa kike, atalainika tu!” alisema Maria huku akiwa na uhakika kwamba Keith kwake, alikuwa hapindui.
Wakaondoka mpaka hotelini, huko, wakajifungia chumbani na kushikanashikana kitandani. Japokuwa alikuwa amefanya mambo mengi ya kishoga lakini kitandani hapo Fareed alikuwa hatari, alikuwa na ujanja mwingi wa kumchezea mwanamke.
Kila wakati Maria alikuwa akiguna kimahaba tu, kwake, kwa mchezo aliokuwa akimuonyesha Fareed haikuwa ya kawaida, ilikuwa michezo hatari ambayo kwa watoto wa kisasa Bongo wangesema si michezo ya nchi hii.
****
Hakukuwa na mtu aliyekuwa akijua kile kilichotokea ndani ya piramidi, watu waliendelea kuingia na kutoka kwa siku hiyo lakini baada ya saa mbili, sauti na mwanamke ikasikika kutoka ndani, kila mtu alishtuka, mbali na kupiga kelele hizo, akatoka huku akihema kwa nguvu.
Kila mtu alimwangalia, alionekana kuona kitu cha ajabu ndani ya piramidi hilo. Polisi na wasimamizi wakamfuata na kumuuliza kilichokuwa kimetokea, akawaambia kwamba aliona maiti ya mtu mmoja ndani ya piramidi lile kitu ambacho polisi na wasimamizi walikataa lakini wakataka kwenda ili kuhakikisha kwa macho yao.
Wakaelekea huko, kile walichoambiwa ndicho walichokiona, waliuona mwili wa mwanaume ukiwa chini, ulichomwa kisu huku ukiwa umeburuzwa na kuacha michirizi ya damu sakafuni. Picha iliyoonekana iliwaogopesha.
Kutokana na mwanga hafifu uliokuwa humo wakashindwa kumgundua mara moja hivyo kuchukua tochi na kummulika, napo hawakumgundua lakini baada ya kuona kadi zake za kibiashara ndipo wakagundua kwamba mtu huyo alikuwa Keith, bilionea mkubwa.
“Ni Keith! Yule bilionea wa Marekani!” alisema jamaa mmoja huku akionekana kushtuka.
“Unasemaje?”
“Si unamuona!”
Hawakujua ilikuwaje mpaka mwanaume huyo kuuawa ndani ya jengo hilo kubwa. Walibaki wakiulizana, alivyoonekana ni kwamba hakuuawa muda mrefu uliopita kwani hata michirizi ya damu ile haikuwa imeganda, ilikuwa damu mbichi kabisa hali iliyoonyesha kama wangeamua kumtafuta muuaji, hakuwa amefika mbali.
Wakaondoka na kuelekea nje, katika geti la kuingilia, walitaka kufahamu mwanaume huyo aliingia na nani ndani ya piramidi lile. Wakapitia majina na kugundua kwamba aliingia na mwanamke aliyeitwa kwa jina la Maria Ogabugu.
“Yupo wapi?” aliuliza jamaa mmoja.
“Hebu tukaangalie kwenye kamera!”
Hilo ndilo walilolifanya, wakaenda katika chumba kilichounganishwa na kamera ndogo za CCTV zilizokuwa mahali hapo, walitaka kuona tangu kipindi watu hao walipoingia, na kama mwanamke huyo alikimbia, ilikuwaje?
Wakafanikiwa kuona kila kitu, tangu alipoingia na mwanaume huyo lakini kilichowashangaza ni kwamba wakati wa kuondoka, aliondoka na mwanaume mwingine, walitamani kumfahamu lakini walishindwa kwa kuwa alivalia kofia kubwa ya Marlboro.
“Ni nani huyu?” aliuliza polisi mmoja.
“Hatujui!”
“Kitu cha kwanza ni kumtafuta huyu mwanamke tutajua tu!” alisema polisi mmoja.
Hakukuwa na muda wa kupoteza, wakaanza kumtafuta katika hoteli mbalimbali. Walijua kwamba kama hilo lilikuwa jina lake basi ni lazima angekuwa ameliandikisha katika hoteli aliyokuwa amefikia hapo Cairo.
Baada ya saa kadhaa, wakagundua kwamba mwanamke huyo alikuwa katika hoteli moja hapo Cairo, wakaanza kufuatilia huko kutaka kujua kama alikuwepo. Walipofika, wakaelekea mpaka mapokezini ambapo wakaulizia na kuambiwa kwamba alikuwepo ndani na mwanaume mwingine hivyo kwenda huko.
“Cha kwanza ni kuwakamata wote wawili, ikishindikana basi tuwapigeni risasi,” alisema polisi mmoja kwani kwa kile kilichotokea, kilikuwa aibu kubwa.
****
Wote walichoka hoi, Fareed alimwangalia Maria, hakummaliza. Hakuwahi kukutana na mwanamke kimwili, huyo ndiye alikuwa mwanamke wake wa kwanza. Alijisikia kuwa na nguvu kubwa, alijua kucheza na mwanamke, alijua maeneo ambayo yangemtetemesha mwanamke yeyote yule.
Maeneo hayohayo ndiyo aliyoshughulika nayo, alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, Maria alipagawa, alikuwa hoi huku akidiriki kusema kwamba kwa kile alichokuwa amekifanya Fareed, hakuwa amefanyiwa na mwanaume yeyote yule.
Fareed akasimama na kwenda kuoga, bafuni, alikuwa na wasiwasi, alihisi kabisa kwamba inawezekana polisi wangefika katika hoteli hiyo kwani alipokuwa ameingia ndani ya hoteli ile, kamera zilimuona na kumgundua kwamba alikuwa nani.
Alifikiria kutoroka siku hiyohiyo, hakutaka kulala mahali hapo, ili maisha yake yaendelee kuwa salama na akamilishe kazi zake zote ilikuwa ni lazima kutoroka hapo hotelini haraka iwezekanavyo kabla mambo hayajaharibika.
Alioga harakaharaka, alipomaliza, akatoka na kuelekea kitandani. Akamshika kiuno Maria na kuanza kukipapasa, hakuishia hapo, akaupeleka mdomo wake katika kiuno kile na kuanza kukifanyia utundu.
Maria akaanza kutoa miguno ya kimahaba, Fareed alifanya hivyo kwa lengo la kumpagawisha halafu amuache, akamvutia kwake, akaupeleka ulimi wake katika kitovu cha msichana huyo na kuendelea kumfanyia utundu huku mikono yake ikitalii katika kifua chake.
Maria alichanganyikiwa, alijiona akiwehuka, akaondoka katika ulimwengu halisi na kuingia katika ulimwengu ambao haukuwepo kabisa ulimwenguni. Fareed hakuacha, aliendelea kwa dakika tatu kisha akamuacha Maria na kumwangalia machoni.
“Endeleaaaaaaa…” alisema Maria huku akimvuta Fareed juu yake.
“Nenda kaoge kwanza!”
“Jamaniiiiiii!”
“Leo mimi ni wako! Yaani hapa huchomoki,” alisema Fareed huku akiupitisha mkono wake shingoni mwa msichana huyo, akakichukua kidole chake cha mwisho na kukiingiza sikioni mwa Maria.
“Ishiiiiii..aagghhuu..” alilalamika Maria kimahaba.
“Nenda bafuni kwanza!” alisema Fareed.
Japokuwa alikuwa amezidiwa lakini hakutaka kupingana na Fareed, hapohapo akasimama na kwenda bafuni kuoga. Huku nyuma Fareed akavaa nguo harakaharaka, alipomaliza, akachukua kibegi chake, akaufungua mlango na kutoka.
Alitaka kushuka kwa kutumia ngazi lakini aliona kama angechelewa, hivyo alichokifanya ni kupanda lifti. Wakati yeye akishuka kwenda chini ndiyo muda ambao polisi walipanda kwenda juu, yaani kwa kifupi, walikuwa ndani ya lifti mbili tofauti na walikuwa wakipishana kwa wakati mmoja.
****
Lifti ikashuka mpaka chini, Fareed hakutaka kubaki mahali hapo, kile kilichomfanya kujenga urafiki na Maria alikikamilisha na hivyo alitaka kuondoka hapo haraka iwezekanavyo.
Alipofika chini, akaanza kutembea kwa mwendo wa kawaida, hakutaka kuonekana kuwa na wasiwasi kwa kuamini kwamba kama angekuwa katika hali hiyo ingekuwa rahisi kwake kukamatwa hata na walinzi waliokuwa katika hoteli hiyo.
Hakukuwa na polisi mapokezini kitu kilichomfanya kutembea kwa uhuru mpaka nje ambapo akachukua teksi na kuondoka mahali hapo. Moyo wake ulikuwa na furaha tele, alifanikiwa kwa kile alichokuwa amekipanga na kitu alichokifikiria kwa kipindi hicho ni kumuua bilionea Belleck ambaye hakujua alikuwa wapi ila kama angekwenda katika ofisi yake moja iliyokuwa nchini Marekani, angejua mahali alipokuwa kipindi hicho.
Akaondoka na kwenda kuchukua chumba katika Hoteli ya Red Dragon iliyokuwa hapohapo Cairo ambapo alipanga kukaa kwa usiku mmoja na kesho kuondoka kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kuanza harakati zake za kutaka kumuua bilionea huyo ambaye alitaka kumuua kipindi cha nyuma ila hakufanikiwa katika hilo.
Hakuchukua muda mrefu akafika katika hoteli aliyokuwa akienda. Akachukua chumba na kwenda kupumzika. Siku hiyo hakupumzika kwa raha, alikuwa akifikiria safari yake lakini cha zaidi ni kwamba alikuwa akifikiria hali ilivyokuwa ikiendelea.
Aliamini kwamba Maria angewaambia polisi kile kilichokuwa kimetokea, angetoa siri kwamba si yeye aliyefanya mauaji bali ni Fareed jambo ambalo lingemuweka kwenye wakati mgumu kwamba hata kusafiri asingeweza kutokana na ulinzi ambao ungewekwa kila kona.
Hakutaka kuona akizuiliwa kusafiri, ilikuwa ni lazima kuondoka na hata kama ingeshindikana kuondoka kwa kupitia uwanja wa ndege, basi angetumia hata meli lakini mwisho wa siku afanikiwe kuingia nchini Marakani.
Akapumzika huku akiwa na mawazo tele, ilipofika majira ya saa kumi jioni, akafungua televisheni na kuanza kuangalia. Habari kubwa ilikuwa ikipita ikionyesha kwamba kulikuwa na mtu alimuua Bilionea Keith kwenye piramidi lililopo Giza.
Moyo wake ukafurahia zaidi lakini akashtuka baada ya kuona picha zile alizokuwa amepigwa kwa kamera za CCTV zikionyesha kwamba muuaji alikuwa yeye na binti mmoja ambaye alikuwa akishikiliwa na polisi.
Moyo ulimlipuka, hakuamini alichokuwa amekiona, mapigo ya moyo yalikuwa yakimdunda kwa nguvu kwa kuamini kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake, kama picha zake zilianza kuwa maarufu kwenye luninga, basi ilikuwa ni lazima atafutwe, atakapoonekana, basi akamatwe.
“Hapa napo si salama kabisa,” alisema Fareed huku akiwa ndani ya chumba kile.
Akafunga mlango kwa ufunguo, akatulia huku akifikiria ni kwa jinsi gani angeondoka ndani ya hoteli hiyo. Ilipofika majira ya saa moja usiku, akasikia sauti za watu kutoka nje.
Haikuwa kawaida kwenye hoteli kubwa kama hiyo, akachungulia chini kupitia dirishani, alichoweza kuona ni kundi la polisi waliokuwa na bunduki wakiwa wamefika hotelini hapo na walikuwa wakiwasisitizia wafanyakazi waruhusiwe kuingia ndani ya vyumba vya hoteli hiyo.
“Mungu wangu! Wamejuaje kama nipo humu?” alijiuliza, hakupata jibu. Hakujua ni kwa jinsi gani angeondoka ndani ya hoteli hiyo, alibaki akitetemeka kwa hofu kubwa kwani kule chini ambapo ndiyo kulionekana kuwa rahisi kwake, pia kulikuwa na polisi.
“Nifanye nini? Mungu nisaidie,” alisema huku akiwa hajui ni kitu gani alitakiwa kufanya.
****
Maria alioga haraka sana, mwili wake uliwehuka, Fareed alimchanganya kupita kawaida, hakukuwa na kitu kingine alichokifikiria mahali hapo zaidi ya ngono tu. Alijisugua hasa, kuanzia chini, kati mpaka juu kuhakikisha mtoto wa kike anakuwa msafi.
Alipomaliza, akachukua taulo lake na kuanza kujifuta, tena huku akihakikisha anakausha maji ya kila sehemu. Alipohakikisha kila kitu kipo sawa, akaufungua mlango wa bafu na kutoka.
Chumbani hakukuwa na mtu, alijaribu kumwangalia Fareed huku na kule lakini hakuweza kumuona sehemu yoyote ile. Hakujua mwanaume huyo alikwenda wapi, mara ya kwanza alihisi kwamba inawezekana aliamua kufuata chakula chini, hakutaka kumsumbua mhudumu lakini kitu cha ajabu kabisa, hata kibegi chake kidogo hakikuwepo chumbani humo.
“Mmmh!” aliguna.
Akaanza kumuita mwanaume huyo chumba humo, hakusikia kitu chochote, hakumuona, akaufungua mlango na kutoka ndani ya chumba kile. Akaanza kuwa na hofu, akahisi kulikuwa na mtu aliingia ndani ya chumba hicho na kumteka mpenzi wake huyo.
Akarudi chumbani na kuanza kuvaa nguo zake harakaharaka lakini hata kabla hajamaliza, akasikia mlango ukianza kugongwa kifujofujo hali iliyomfanya kuwa na hofu.
“Nani?” aliuliza kwa sauti.
“Fungua mlango!” alisikika mwanaume aliyekuwa nje ya chumba kile.
ITAENDELEA SIKU YA KESHO HAPA HAPA
Kama ulipitwa na sehemu za nyuma soma hapa zipo zote Bonyeza >>>www.2jiachie.co.tz/search/label/Simulizi?&max-results=10
Post a Comment