ad

ad

Askofu Ashangaza Wengi Kuruhusu Pombe Kanisani


Askofu Tsiets Makiti wa Afrika Kusini akionyesha pombe.
HATUA ya Askofu Tsiets Makiti wa Afrika Kusini, kuruhusu unywaji wa pombe kanisani si tu imeshangaza, bali imeshtua watu wengi.
asko
Jina hilo ni la kilugha huko Afrika Kusini likiwa na maana ya kanisa la wanywaji ama walevi. Sehemu ya kuuzia bia (Counter) ipo ndani ya kanisa hilo.
Wakati wa ibada, askofu Makiti huonekana altareni amevalia kofia ya kiaskofu na msalaba shingoni na mbele yake kukiwa na chupa kadhaa za bia na pombe kali.
Baadhi ya picha zilimwonesha akiwa ameweka lita 4.5 za pombe kali na chupa nyingine za bia mbele ya altare.
Wakati ibada ikiendelea Askofu Makiti huonekana akichukua glasi na kumimina bia ili kukata kiu.
“Tunakaribisha walevi wengine kutoka makanisa mbalimbali. Lengo la kanisa langu ni kuweka mazingira mazuri ya kuwavuta wateja wa pombe ambao wanaandamwa kwenye makanisa yao.
“Hapa kanisani tunakunywa bila kificho na kumsifu Mungu, si utani… tunatoa nafasi kwa watu kumrudia Mungu bila kujali ni walevi au la,” anasisitiza.

Anasema watoto na vijana hawataruhusiwa kabisa kugusa kinywaji cha aina yoyote kwani ni kwenda kinyume cha malezi yao.
“Hili la unywaji linahusu wanaume watu wazima tu kwa sababu hata wanawake hawaruhusiwi kabisa,” anasema Askofu Makiti.

Akitilia mkazo suala hilo, anasema; “Popote tutakapokuwa na ibada hatutaruhusu watoto kununua pombe hata kama wametumwa na wazazi wao, tutawarudisha,” alisema nia ya kanisa lake ni kuwakusanya wale wote waliotengwa kwenye dini zao kwa sababu ya ulevi.

Muumini mmoja wa kanisa hilo, aliwaacha wenzake wakivunjika mbavu baada ya kupiga mwereka wakati akijongea kaunta kuchukua bia.
Wakati tukio linatokea waumini wenzake walisika wakisema kwa sauti “gabola!” ikiwa na maana ya walevi.

Kama hiyo haitoshi, muumini mwingine aliwaacha wenzake wakiangua kicheko baada ya kuangusha chupa ya bia na kupasuka.
Baada ya kitendo hicho kutokea, mhusika alisogea taratibu bila kuzungumza na mtu na kwenda kujibanza pembeni mwa ukuta.
Wakati hayo yakitokea, waumini wengine walikuwa wakiserebuka baada ya pombe kupanda kichwani huku wakionekana wenye macho ya kulegea.
Nyimbo zao nyingi zinahusu masuala ya dini na mikononi hushikilia chupa za bia huku wakiburudika taratibu ambapo humvutia sana Askofu Makiti.

“Nina furaha mno siku ya leo kuwa miongoni mwa waumini wa Kanisa la Gabola, inafurahisha sana,” anasema mmoja wa waumini.
Kwa mujibu wa Askofu Makiti, zaidi ya waumini 2, 000 wamejiunga na kanisa hilo na kupatiwa ubatizo.
“Kama unakunywa bia, utabatizwa kwa bia,” anasema na kuongeza kuwa kanisa hilo limeleta mabadiliko makubwa kwa waumini wake.
“Huwezi kuona waumini wakifanya vitendo vya ovyo hata wakati wanakunywa pombe. Ni wastaarabu. Hata vitendo vya uhalifu vimepungua,”anasisitiza.

Anasema kanisa lake limekuwa mfano mzuri kuliko mengine kwani yanayoendelea huko yanasikitisha kwani taarifa zao husikika katika vyombo vya habari.

“Makanisa mengine tunasikia wanavuta mafuta ya petroli na kula majani, kama hivi ndivyo cha ajabu kwenye kanisa langu ni kipi?” anahoji.
“Tunachofanya sisi ni kunywa, kumsifu na kumtukuza Mungu. Hakuna kingine zaidi hicho na hakuna anayetumia nguvu za giza,” anafafanua.
Askofu Makiti anaongeza kuwa, “jambo ninalotaka tuelewane hapa ni kwamba tusihukumiwe kwa sababu ya kunywa pombe”.
Makiti anasema mipango yake ya baadaye ni kuhakikisha anafungua matawi zaidi maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ili aweze kujipatia waumini.
“Tumepata mialiko mingi kutoka kwa watu mbalimbali wakituomba tufungue Kanisa la Gabola huko walipo, kwa hiyo hivi karibuni tutakwenda kaskazini magharibi mwa nchi kwa kazi hiyo,” anasema.
Wakati wa ibada waumini wake ambao wengi ni wanaume huonekana wamekaa chini wakimsikiliza anapotoa mahubiri wakiwa na bia zao, ambapo husikika wakisema “Ameni au Gabola”
“Acha tutumie fedha zetu kwa sababu ni zetu, acha tufurahie na kusapoti wauzaji…nendeni huko muwaambie walevi wote waje Kanisa la Gabola kwa sababu ufalme wa Mungu upo,” alisema wakati akitoa mahubiri yake.
“Msihofu chochote eti kwa sababu mnakunywa pombe. Kwa hiyo msiogope kwa sababu kwenye Kanisa la Gabola kuna kila kitu kwani ninyi ni wana wa Mungu,” anasema.

No comments

Powered by Blogger.