MADAI MAZITO: Msanii Lulu Diva Apewa Jeep na Nyumba na Kigogo!
KAUNTA ZA VINYWAJI Ndani ya mjengo huo una kaunta mbili maalum kwa vinywaji laini ambapo ya kwanza ipo sebuleni na ya pili ipo jikoni huku pia kukiwa na friji kubwa la kisasa la milango miwili lenye thamani ya mamilioni.
SEBULE YA KISASA Ukiachana na sofa na fanicha za kisasa, upande wa sebuleni umepambwa kwa ‘wallpaper’ za aina yake sambamba na nakshinakshi kwenye meza maalum iliokaa mfano wa ‘dressing table.’
ENEO KUBWA LA PARKING Upande wa nje kuna eneo kubwa la parking la kisasa lililo ndani ya uzio ambapo eneo hilo unaweza kuhifadhi magari zaidi ya matano.
GARI LA KIFAHARI Ukiachilia mbali ndani na nje ya jumba hilo, Lulu Diva pia anamiliki gari jeusi la kifahari aina ya Jeep ‘Liberty’ toleo la Marekani.
AMETOA WAPI JEURI? Licha ya kuendelea kusumbua na kuwa msanii mwenye mafanikio kwa sasa, Lulu ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva walioanza rasmi muziki mwaka jana akiwa ameshikilia ngoma tatu hadi sasa, Usimuache, Utamu na Give It To Me. Awali alikuwa akiuza sura kwenye muziki huo, swali la kujiuliza amepata wapi jeuri hii? Katika kumdodosa, Lulu Diva amesema ana siri nzito kuhusu maisha yake bomba anayoishi sasa hivyo akaomba subira kabla ya kumuanika anayempa jeuri mjini. https://www.youtube.com/c/KidaniStars
Post a Comment