Baada
ya Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa kumtembelea Rais Magufuli Ikulu
Leo January 9, 2018 Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye yupo
nchini Ubelgiji kwa ajili ya matibabu ametoa mtazamo wake kuhusu suala
hilo
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lissu amepost picha inayomuonesha Lowassa akiwa Ikulu na kuandika maelezo haya; “Na hatukatai kuzungumza na Magufuli kuhusu matatizo mengi na makubwa yanayoikabili nchi yetu.”
“Lakini
ni muhimu na lazima viongozi wakuu wa chama washirikishane na
washauriane kabla ya mazungumzo hayo. Na baada ya mazungumzo, ni lazima
viongozi wakubaliane juu ya kauli za kutoa hadharani kwa umma ili wote
tuwe kwenye ukurasa mmoja.
“Viongozi
na wanachama wetu wanashambuliwa hadharani kwa mapanga na hata kwa
risasi, kumsifia Rais ni kumuunga mkono yeye. Katika mazingira ya kesi
nyingi za kutunga dhidi yetu, ‘kazi nzuri’ inayofanywa ina maana gani,
kama sio kuhalalisha ukandamizaji tunaofanyiwa.
“Katika
mazingira ambapo hata jumuiya ya kimataifa imeanza kuhoji mwenendo wa
Rais Magufuli, kutoa kauli kwamba ‘anafanya kazi nzuri’ ni ‘kumtupia
taulo’ la propaganda litakalomfichia madhambi mengi aliyowafanyia
Watanzania katika miaka hii miwili.
“Kwa vyovyote vile, kitendo cha Lowassa sio cha kunyamaziwa au kuhalalishwa kwa hoja nyepesi nyepesi.”– Lissu
1: Waheshimiwa habari za Tanzania na poleni kwa yote. Naomba na mimi niseme kwa uchache kuhusu suala la Mheshimiwa Lowasa. Baada ya Mwenyekiti kuzungumzia jambo hili, inaelekea kuwa wazi kwamba Mheshimiwa Lowassa hakumshirikisha Mwenyekiti kabla ya kukubali au kuamua kwenda Ikulu kukutana na Rais Magufuli. . Na juzi tu wakubwa wetu hawa wawili walikuwa pamoja hospitalini kumsalimia Mzee Ngombale Mwiru. . Je, inawezekana Mheshimiwa Lowassa hakuwa anajua tayari kwamba ana appointment Ikulu? Kama alikuwa anajua, kutokumshirikisha Mwenyekiti wake kuna tafsiri gani hasa? Katika mazingira ya sasa ya Tanzania ya Magufuli, uamuzi wowote wa kufanya nae mazungumzo, hata kwa nia njema yoyote ile, bila kushauriana au kuwashirikisha viongozi wa juu wa chama, ni uamuzi usio sahihi na mgumu kukubalika. . Vile vile, kauli za aina ambayo tumeisikia leo kutoka kwa Mheshimiwa Lowassa, zina athari kubwa kisiasa. . Sio tu zinachanganya wanachama na wafuasi wetu, lakini pia zinawapa mtaji wa kisiasa maadui zetu. . Kuanzia sasa tutegemee sana kuwasikia maCCM yakishangilia 'busara' za Mheshimiwa Lowassa. . Masuala ya ukiukwaji haki za binadamu, uvunjwaji wa Katiba na mengine mengi sasa yatajibiwa kwa namna moja: Lowassa amemkubali Magufuli nyie wengine mnapiga kelele za nini. . Huu ni mtaji wa bure kwa Magufuli. Ukweli, ambao umesemwa sana humu, ni kwamba amefeli karibu katika kila jambo. . Hata hiyo reli anayosifiwa nayo na Lowassa bado ni ndoto tu: nani ajuaye itajengwa kwa hela za nani??? . Za Wachina kama tulivyoambiwa mwanzoni; au za Waturuki kama tulivyoambiwa baadae; au za Afrika Kusini kama alivyosema mwenyewe anaenda kumwomba Zuma??? . Kama chama hatujawahi kukataa mazungumzo na Rais au kiongozi mwingine yeyote wa serikali. Itaendelea .....
Post a Comment