DAWASCO yakubali kulipa fidia Nyumba Iliyoungua Moto
Mamlaka
ya maji safi na maji taka jijini Dar es salaam DAWASCO imesema itamlipa
fidia mmiliki wa nyumba iliyoungua moto jana maeneo ya Buguruni
kutokana na moto uliosababishwa na shughuli za mamlaka hiyo.
Akiongea
kwenye eneo la tukio Mkurugenzi mtendaji wa DAWASCO Mhandisi Cyprian
Luhemeja amesema ofisi yake inaongea na mmiliki huyo ili kuona namna ya
kumlipa kutokana na uharibifu uliotokea.
''Tunaongea
naye kuona jinsi gani tutamlipa fidia kwa uharibifu huu uliotokea ili
aweze kuendelea na maisha yake na familia kama kawaida'', amesema
Luhemeja.
Kwa
upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala Salum Hamduni
amesema zoezi la kuziba bomba la gesi la Songasi ambalo liliungua juzi
usiku limefanikiwa na hali kwa sasa ni shwari baada ya kufanikiwa kuziba
'valve' zilizopasuka.
Tukio
hilo la moto lilitokea juzi jioni katika eneo hilo la Buguruni Mnyamani
baada ya mafundi wa DAWASCO kupasua kwa bahati mbaya bomba la gesi la
Songasi ambalo lilisababisha kulipuka kwa moto huo.
Post a Comment