CCM yamjibu Askofu Kakobe baada ya kuikashifu serikali
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam,
Frank Kamugisha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni
siku moja baada ya Aksofu Kakobe kukosoa namna serikali inavyotenda
mambo yake, akisisitiza kwamba Tanzania si nchi ya chama kimoja kama
ambavyo viongozi wanataka kuigeuza na hivyo kuwataka viongozi wa
serikali waanze kutubu.
Kamugisha
amesema kuwa, wao kama viongozi wa CCM hawaweza wakakaa kimya wanapoona
chama kinachafuliwa na viongozi wake ambao wanafanya kazi kwa niaba ya
watanzania wakikashifiwa.
Aidha,
alisema kuwa, siasa ni kwa ajili ya wanasiasa, na kama kiongozi wa dini
ana jambo lolote analotaka kuzungumzia, kuna busara za kutumia na sio
kutumia kanisa kusema hayo.
Post a Comment