Serikali Yaanza Kuwashughulikia Wasanii Wanaovaa Nusu Uchi
Waziri
wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amesema
wizara imeanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli juu ya baadhi ya
wasanii ambao wanadaiwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili ya
kitanzania.
Waziri
Mwakyembe ametoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa
habari na kusema kwamba kitendo cha Rasi Magufuli kusema suala hilo,
kimewapa nguvu ya kuzidi kupambana na wasanii, ambapo hapo awali
walikuwa wakiwagusa huwajia juu na kulalamika.
"Pale
tunapoona kuna ukiukwaji, tufumbe macho tusijali malalamiko yanavyokuja
kutolewa, maana ukiwagusa wasanii walikuwa wanakuja juu sana, lakini
tunashukuru mkuu wa nchi kulisemea hilo, basi na sisi tumeongezewa nguvu
basi hatutaachia suala hilo kuendelea kuharibu vizazi vyetu", amesema
Waziri Mwakyembe.
Hivi
karibuni Rais Magufuli alizitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua
wasanii wanaovaa nusu utupu kwenye kazi zao za sanaa ambazo zingine
huonyeshwa kwenye television, ambazo amedai hazina maadili na
zinadhalilisha utamaduni wetu na kuharibu kizazi kijacho.
Post a Comment