MCHEKESHAJI maarufu Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amefungukia madai yaliyokuwa yakiwatafuna wasanii wa Bongo Movies kuwa wamemtenga muigizaji mwenzao, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na kusema kuwa, hawajamtenga bali hawakutegemea kama mambo yangefika yalipofika.
Steve alisema, wasanii wengi wa Bongo Movies hawakuonesha kama wameguswa sana na matatizo ya Lulu aliyehukumiwa miaka miwili jela kwa kosa la kuua bila kukusudia, kwani hawakutegemea kama lingefikia kwenye hatua hiyo.
“Si kwamba tulimtenga hapana, unajua watu wengi hatukutegemea kama kesi hii ingefika kwenye hatua ya Lulu kufungwa, tuko pamoja naye tunajipanga kama wasanii kuona namna ya kumfariji mama Lulu katika kipindi hiki kigumu,” alisema Nyerere.
Post a Comment