Ester Kiama Mapedeshee wa Kuwarubuni Mastaa Bongo Wamepitwa na Wakati
Msanii wa filamu Bongo Ester Kiama.
MSANII anayekuja vizuri kupitia tansia ya filamu Bongo Ester Kiama amefunguka kuwa, wale waliokuwa wakijinasibu kuwa ni mapedeshee na kuwarubuni mastaa mbalimbali sasa hivi wamepitwa na wakati (zilipendwa) kwa kuwa vyuma vimekaza.
Ester alisema kuwa mastaa wengi wamegundua mapedeshee hao kwa sasa wamefulia na hawakuwa na mapenzi ya kweli kwao, zaidi ya kutaka kuwatumia kutokana na umaarufu walionao ili kufurahisha mioyo yao na kujisifu kwa watu wao wa karibu.
“Unajua zamani mapedeshee walikuwa wakitumia mifuko yao kuwarubuni mastaa mbalimbali lakini sasa mambo yamebadilika, hata mastaa nao wamebadilika wengi wao hawatazami pesa bali ni mapenzi ya dhati,” alisema Ester.
CREDIT: GPL

Post a Comment