Apple kuinunua Beats
Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3
Kampuni kubwa ya teknolojia
Apple imethibitisha kwamba itanunua vipokea sauti na huduma ya
kusikiliza muziki kupitia kwenye mtandao wa inteneti kutoka kampuni ya
Beats Electronics katika makubaliano ya dola bilioni 3.
Hayo yakiwa ni makubaliano makubwa katika historia ya miaka 38 ya kampuni hiyo.Hatua hiyo inaonekana kama jitihada ya kuiendeleza sifa ya Apple katika soko la kusikiliza
muziki kwenye mtandao.
Pamoja na ununuzi huo, waanzilishi wa Beats Jimmy Lovine na msanii mtajika katika mtindo
wa kufoka na Hip Hop Dkt. Dre watajiunga na kampuni hiyo ya kiteknolojia.
Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3
Beats ilianzishwa na mzalishaji wa muziki Jimmy Lovine na nyota wa mziki wa kufokafoka, Dr. Dre, na mitambo hiyo imejulikana kuwa bora zaidi hadi siku za hivi majuzi.
Beats ilianzisha huduma ya muziki unaolipiwa mapema mwaka huu.
Apple ina huduma ya iTunes ambayo ndio kubwa zaidi duniani inayohusiana na mziki, na ilianzisha kituo cha radio cha iTunes mwaka uliopita.
Apple kuinunua Beats kwa dola bilioni 3
mfumo
wa dijitali, imekuwa ikikumbwa na ushindani mkubwa kutoka kwenye huduma zinazolipiwa
kama vile Spotify, Pandora na Rdio.
Hata hivyo, huduma ya mziki ya Beats ina wateja wapatao 110,000 pekee waliojisajili
ikilinganishwa na Spotify ilio na watu milioni 10 waliojisajiliwa.
Mkataba huo na kampuni ya Beats imeonyesha kudidimia kwa Apple ambayo hujulikana kwa
kutengeneza bidhaa mpya wala sio kununua kampuni ndogo ndogo kama wanavyofanya
wapinzani wao Google.
Post a Comment