ad

ad

Kifo Cha Ndikumana Chaiachia Majonzi Soka Rwanda

Aliyekuwa Kocha Msadizi wa Rayon Sports, Hamad Ndikumana (katikati) alipokuwa akiongoza mazoezi ya wachezaji wa timu hiyo.

KIFO cha Hamad Ndikumana, aliyekuwa maarufu zaidi nchini mwake Rwanda kama Katauti, kimeombolezwa kwa wimbi kubwa la huzuni miongoni mwa watu wa Rwanda hususani katika duru za michezo. Rais wa Chama cha Soka cha Rwanda (FERWAFA) Vincent Nzamwita, amesema nchi imepoteza mtu mashuhuri aliyependa soka na aliyeipenda nchi yake.

Katauti alistaafu rasmi kucheza soka mwaka 2015 na kuwa kocha wa Espoir Football Club.  Msimu uliofuata aliutumia kama msaidizi wa kocha wa Musanze FC, chini ya mchezaji mwenzake wa zamani wa  Rayon,  Sosethene Habimana.

Katauti  aliyeacha watoto wawili aliichezea timu ya taifa ya Rwanda (Amavubi) kwa zaidi ya miaka 10 ambapo umahiri wake katika soka ulimfanya kuwa kapteni wa timu hiyo.
Hamad Ndikumana Alianza kucheza soka mnamo miaka ya 1990 nchini Burundi kabla ya kuhamia Rwanda kisha akaelekea Ubelgiji na Cyprus.
Akiwa bado kijana, alicheza mechi kadhaa za shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) na Ligi ya Uropa.
Klabu alizochezea Katauti

Miaka              Klabu                     1998–1999     Rayon Sports  (Rwanda)   2000–2001     KV Turnhout   (Belgium)   2001–2002    RSC Anderlecht  (Belgium)   2002–2003    KV Mechelen    ((Belgium)   2003–2005    KAA Gent    (Belgium) 2005–2006   APOP Kinyras Peyias FC (Cyprus) 2006–2007   Nea Salamina     (Cyprus) 2007–2008   Anorthosis Famagusta FC (Cyprus) 2008–2009   AC Omonia   Nicosia (Cyprus)      2009–2010   AEL Limassol  (Cyprus)  2011               APOP Kinyras Peyias FC (Cyprus)
Timu ya Taifa Nahodha wa timu ya Rwanda 1998

No comments

Powered by Blogger.