Hukumu Ya Lulu Yamshangaza Diana Kimaro
MSANII wa filamu Bongo Diana Kimaro amesema kuwa, hukumu ya msanii mwenzake Elizabeth Michael ‘Lulu’ imemshangaza kwa kuwa hakutegemea kama mwanadada huyo atapelekwa mahabusu na kujikuta akikesha kumuombea.
Akibonga machache na paparazi wetu shosti huyo wa Lulu alisema, jambo hilo limemuumiza mno kwani alitegemea hukumu nyepesi tofauti na hiyo iliyotolewa, hata hivyo hana cha kufanya zaidi ya kukesha akimuombea kwa kuwa anaamini ipo siku Mungu atatenda muujiza wake akatoka kabla muda huo haujaisha.
“Sikuwaza kabisa kama muda huu tunaoongea Lulu usingizi wake anaupata Segerea, kiukweli nimeumia mno hili jambo limenipa mstuko mkubwa hadi sasa sipo sawa, kimbilio la mwisho ni Mungu tu,”alisema kwa majonzi.
Post a Comment