Tume ya uchaguzi IEBC yaahirisha uchaguzi wa wa leo tarehe 28 magharibi mwa Kenya
Tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC imetangaza kuhairishwa kwa uchaguzi wa urais ambao ulitarajiwa kuandaliwa tarehe 28 mwezi huu katika kaunti nne magharibi mwa Kenya yaliyo kwenye ngome ya upinzani.
Kaunti hizo ni pamoja Migori, Siaya, Kisumu na Homa Bay.
Uchaguzi huo ulihairiswa kwa sababu za kiusalama maeneo hayo wakati wafuasi wa upinzani wakipinga kufanyika marudio ya uchaguzi
Katika taarifa yake Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema kuwa tume imechukua hatua hiyo ili kulinda maisha ya wafanyakazi wake
Odinga kutangaza hatua ya kuchukua Jumatatu
Bw Odinga amewaambia wafuasi wake Kibera, Nairobi kwamba atatangaza hatua ya kuchukua Jumatatu.
Odinga: Tutakarabati shule maeneo yaliyoharibiwa
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametembelea mtaa wa Kibera ambapo amesisitiza kwamba upinzani hautalegeza msimamo wake.
Amesema shule mbili ambazo ziliharibiwa wakati wa makabiliano ya wafuasi wake na polisi jana wakati wa uchaguzi zitakarabatiwa.
Amesema shule mbili ambazo ziliharibiwa wakati wa makabiliano ya wafuasi wake na polisi jana wakati wa uchaguzi zitakarabatiwa.

Post a Comment