Miaka 18 Hayati Mwalimu Nyerere Atakumbukwa Kwa Juhudi Za Kuimairisha Sekta Ya Utalii Nchini
Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DOdoma
“Uhai
wa wanyamapori ni jambo linalotuhusu sisi sote katika Afrika, viumbe
hai wa porini wakiwa katika mapori waishimo sio muhimu tu kwa ajili ya
kuajabiwa na kuvutia lakini pia ni sehemu ya maliasili yetu na
mustakabali wa maisha yetu baadaye”
Hayati
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema hayo wakati akitoa tamko la
Arusha kuhusu Uhifadhi wa wanyamapori kipindi Tanganyika inapata Uhuru
mwaka 1961.
Alisema
kukubali dhamana ya wanyamapori, watanzania wanawajibu wa kufanya kila
liwezekanalo kuhakikisha wajukuu na watoto wa kitanzania wanaweza
kufurahia urithi mkubwa wa thamani hiyo adhimu ya wanyamapori.
Juhudi
za uhifadhi na kulinda rasilimali, malikale na kuendeleza shughuli za
ufugaji nyuki pamoja na kukuza Sekta ya Utalii ikiwa ni jukumu la Wizara
ya Maliasili na Utalii zilikuwepo hata kabla ya ukoloni ambapo jamii
nchini zilitenga mapori kwa ajili ya kuabudia na kutambika.
Kuingia
kwa wakoloni nchini kuliambatana na kutunga Sheria za uhifadhi wa
rasilimali za maliasili na malikale ambapo ni Sheria ya kuhifadhi
Majengo ya kihistoria ya mwaka 1937, Sheria ya Makumbusho ya mwaka 1941,
Sheria ya Usimamizi wa Misitu ya mwaka 1957, Sheria ya Hifadhi ya
Ngorongoro ya mwaka 1959, Sheria ya Hifadhi za Taifa ya mwaka 1959 na
Sheria ya kuhifadhi wanyama ya mwaka 1959.
Chini
ya uongozi wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, kuanzia mwaka 1961
Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa na Sera na Sheria tofauti
kulingana na mabadiliko yaliyokuwa yakitokea duniani katika nyanja za
kiuchumi, kiteknolojia, kiasiasa na kijamii.
Juhudi
za Baba wa Taifa katika kuhakikisha Sekta ya utalii mwaka 1961 ilikuwa
na idara moja ambapo ilianza kuwa na Sera ya uhifadhi wa maliasili,
malikale na kuendeleza utalii nchini.
Mabadiliko
na matukio makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii mara baada ya uhuru
mwaka 1961 yalipelekea jitihada za makusudi za kuwezesha wazawa kielimu
ili kuweza kuchukua nafasi za utendaji na uongozi ambazo awali
zilishikiliwa na wageni.
Aidha,
mwaka 1967 kufuatia kupitishwa Azimio la Arusha mali binafsi
zilitaifisha na kuundwa kwa mashirika na taasisi za umma ambapo Wizara
iliunda mashirika ya umma ikiwemo Shirika la Wanyamapori, Shirika la
Viwanda vya mbao, Shirika la Utalii Tanzania, Shirika la kuhudumia
wasafiri na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kukuza na
kuimarisha sekta ya utalii nchini.
Katika
mabadiliko hayo ndani ya Wizara, juhudi za Mwalimu Nyerere zilipelekea
Serikali kujitoa katika kuendesha shughuli za kibiashara na kujikita
katika kusimamia Sera na uwezeshaji.
Kadhalika
katika suala la ulinzi wa rasilimali za maliasili za taifa, Serikali
ilirithi mfumo wa kikoloni na kuendelea kuwa mlinzi na mwendelezaji mkuu
wa rasilimali za maliasili, malikale na utalii.
Miaka
1991 Serikali ilifanyika mabadiliko ya kisera yaliyokuwa na mwelekeo wa
uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali kwa kuhimiza ushirikishwaji wa
jamii katika uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali za maliasili,
malikale na utalii.
Ushirikishwaji
huu wa jamii katika shughuli za maliasili na utalii ulipelekea Wizara
kuanzisha vitengo mbalimbali ikiwemo kitengo cha Ugani katika idara na
taasisi zake ikiwa na lengo la kuimarisha na kukuza sekta ya utalii
nchini.
Katika
suala la ajira katika wizara wakati nchi inapata uhuru, jinsia
haikupewa kipaumbele katika sekta za maliasili hususani wanyamapori,
misitu, malikale na nyuki. Kazi hizo zilikuwa maalumu kwa wanaume ambapo
juhudi za Mwalimu Nyerere zilipekea mabadiliko ya kimtazamo
uliosababisha kupatikana kwa ajira ikihusisha jinsia zote mbili, ambapo
kwa mara ya kwanza sekta ya utalii iliajiri mwanamke mwaka 1970.
Katika
sekta ya nyuki wanawake wawili waliokuwa na astashahada ya ufugaji wa
nyuki waliajiriwa mwaka 1975, sekta ya misitu iliajiri mwanamke wa
kwanza mwenye shahada mwaka 1976, katika sekta ya wanyamapori mwanamke
aliajiriwa mwaka 1967 na katika sekta ya mambo ya kale mwanamke
aliajiriwa mwaka 1978 kwa ngazi ya cheti na 1981 kwa ngazi ya shahada.
Katika
kuongeza tija na kufanya maamuzi kwa kutumia taarifa zilizofanyiwa
utafiti, wizara ilianzisha vyuo vya ulinzi, uhifadhi na uendelezaji wa
maliasili, malikale na utalii ambapo chuo cha viwanda vya misitu
kilianzishwa mwaka 1975, chuo cha ufugaji nyuki Tabora mwaka 1978 pamoja
na vyuo vya elimu ya wafanyakazi Rongai na Sao Hill vilivyoanzishwa
mwaka 1979 kwa lengo la kutoa elimu ya awali ya uoteshaji miche na
kuhudumia misitu.
Katika
kukuza na kuimarisha sekta ya utalii nchini Mwalimu Nyerere aliweza
kutekeleza majukumu ya wizara kulingana na mabadiliko ambayo yamekuwa
yakitokea nchini na duniani katika nyanja ya kiuchumi, kisiasa
kiteknolojia na kijamii.
Juhudi
hizo zilipelekea wizara kuongeza vituo vya malikale na kutangaza maeneo
tofauti kama urithi wa Taifa, mashamba ya miti yaliongezeka, misitu ya
asili pamoja na hifadhi za Taifa kuongezeka.
Mbali
na juhudi hizo za Mwalimu zilisaidia kukuza na kuimarisha sekta ya
utalii mara baada ya uhuru zilipelekea ongezeko la mikusanyo ya malikale
ambapo wakati wa uhuru wizara ilihifadhi jumla ya mikusanyo ya 10,151
ya fani za Akiolojia, mila, historia, bayolojia na nyaraka mbalimbali.
Aidha,
baada ya uhuru kutokana na tafiti zilizofanywa na watafiti wazawa na
wageni kutoka nje ya nchi hadi juni, 2011 wizara imefanikiwa kuhifadhi
nchini urithi wa malikale unaohamasisha wenye jumla ya mikusanyo
337,361.
Katika
suala la ongezeko la idadi ya watalii wanaongia nchini ndani ya uongozi
wa Mwalimu Julius Nyerere idadi ya watalii iliongezeka kutoka watalii
9,847 mwaka 1960 hadi watalii 103,361 mwaka 1986.
Tukiwa
tunaadhimisha miaka 18 bila Mwalimu Nyerere kumekuwa na mafaniko
makubwa katika sekta ya utalii ambapo mpaka kufikia mwaka 2016 idadi ya
watalii waliotembelea nchini Tanzania ilifika 1,284,279
Ukuaji
huo wa sekta ya utalii unatokana na misingi imara iliyowekwa na Baba wa
Taifa Mwalimu Nyerere kuendelezwa na kusimamiwa kwa manufaa ya sasa na
baadaye.
Post a Comment