ad

ad

Manji Apata Janga Jingine, Apoteza Udiwani



Mfanyabiashara Yusuf Manji amepoteza sifa ya kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu kutokana na kutohudhuria vikao zaidi ya sita na vikao vya kamati vya maendeleo ya halmashauri ya Temeke zaidi ya vitatu.

Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo amesema hayo leo Jumatano katika mkutano na waandishi wa habari.


Kutokana na hilo wamemuondoa Manji kwenye nafasi hiyo kutokana na kukosa sifa.


Chaurembo amesema amemwandikia Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kuhusu suala hilo ili aweze kupanga uchaguzi mwingine.


Chanzo: Mwananchi

No comments

Powered by Blogger.