YANGA YAENDA KUSHITAKI, YADAI KUNA MCHEZO MCHAFU ILI SIMBA IPEWE POINTI ZA BURE
Klabu ya Yanga imetangaza kuwa imeshatoa tipoti juu ya uwepo wa
uwezekano wa wapinzani wao wa jadi, Simba kupewa pointi tatu za bure kwa
upendeleo
licha ya timu yao kufungwa mabao 2-1 ilipocheza dhidi ya Kagera Sugar, wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne kwenye makao makuu ya Yanga mitaa ya Jangwani jijini Dar es Salaam, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Yanga, Salum Mkemi kwa niaba ya kamati yao alisema wanaipinga rufaa ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa madai ya kumchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.
Katika mkutano huo wa waandishi Mkemi pia alikuwa na katibu mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa.
Simba ilikata rufaa kupiga Kagera kumtumia mchezaji Mohammed Fakhi wakidai alikuwa na kadi tatu za njano wakati Kagera wao wanasisitiza alikuwa na kadi mbili za njano na moja ya tatu inayozungumzwa na Simba aliipata katika Kombe la FA ambalo kadi zake hazina uhusiano na mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo ndipo mchezo dhidi ya Simba ulichezwa huko.
Mkemi amesema wameshatoa taarifa kwenye mamlaka husika kadhaa ikiwemo katika mamlaka za mawasiliano ili kuona kama kuna ujanja uliofanyika baina ya watu wa Simba na wajumbe wa Kamati ya Masaa 72 ambayo ndiyo itakayotoa uamuzi huo wa rufaa ya Simba.
Simba na Yanga ndizo zinazoonekana kuwa ubingwa wa msimu huu ambapo Simba ipo kileleni ikiwa na pointi 28 katika michezo 26, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 56 katika michezo 25.
Ikiwa Yanga itashinda mchezo wake wa kiporo maana yake ni kuwa itarejea kileleni na kuicha Simba kwa pointi moja, lakini kama Simba itapewa pointi hizo basi itaiacha Yanga kwa tofauti ya pointi mbili.
Yanga wanasema mchezaji anayekatiwa rufaa amekubali kuwa ana kadi tatu za njano lakini mbili za VPL na moja ni kadi ya FA na hazihusiani hivyo Yanga wanahisi kuwa Simba wanafanya udanganyifu ili wapate pointi za mezani na kuitoa Yanga kileleni.

Post a Comment