Simba Wamtambulisha Mrithi Wa Mayanja Kutoka Rwanda
BAADA ya kupita siku
moja tangu kocha msaidizi wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, raia wa Uganda
aamue kujiweka pembeni kukinoa kikosi hicho, hatimaye uongozi wa timu hiyo
umemalizana na aliyekuwa kocha wa Rayon Sport ya Rwanda, Irambona Masoud Djuma, kwa ajili ya kubeba mikoba ya Mganda huyo.
Akizungumza mbele ya
waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo, Djuma aliweka hadharani kuwa
amekuja katika kikosi hicho kwa ajili ya kufanya kazi na kukisaidia kufanya
vizuri kwenye kila kombe watakaloshiriki.
“Nimekuja hapa Simba kwa
ajili ya kaufanya kazi tu, na nataka tushirikiane ili timu iweze kusonga mbele
itoke hapa ilipo, na pia nipo hapa ili kukuza jina langu maana kiukweli
unapozungumzia Simba unazungumzia juu ya klabu kubwa hapa nchini,” alisema
kocha huyo.
Lakini pia uongozi
wa Simba chini ya Kaimu Rais wake, Salim Abdallah ‘Try Again’, umemteua Richard Robert kuwa meneja wa kikosi
hicho akichukua mikoba ya Cosmas Kapinga ambaye aliamua kubwaga manyanga hivi
karibuni.
Post a Comment