ad

ad

Simba wamtajirisha Ibrahim Ajibu, amwagiwa...

KIWANGO kikubwa alichokionyesha mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu, kimemshawishi mmoja wa mashabiki wa timu hiyo kumkabidhi Sh 300,000 kama pongezi. Ajibu, hiyo ni mechi yake ya pili kucheza dhidi ya Simba akiwa na Yanga aliyojiunga nayo msimu huu wa Ligi Kuu Bara akitokea Msimbazi baada ya mkataba wake kumalizika. 


Nyota huyo, alikionyesha kiwango hicho kikubwa katika mechi ya juzi Jumamosi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar na kumalizika kwa sare ya bao 1-1. Championi Jumatatu lilishuhudia mshambuliaji huyo akikabidhiwa fedha hizo mara baada ya mechi hiyo akiwa kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. 


Katika mechi hiyo, Ajibu hakufanikiwa kufunga bao lakini alionekana kuwa mwiba kwa mabeki wa Simba walioonekana kumchezea rafu mara kadhaa alizokuwa akimiliki mpira. 

Ajibu katika mechi hiyo, alifanikiwa kupiga mashuti mawili pekee kati ya hayo moja lilidakwa na kipa wa Simba, Aishi Manula huku lingine likitoka nje.

 Aidha, Ajibu katika mechi hiyo aliotea mara moja pekee huku akikosa bao kwa tikitaka aliyoipiga akiwa ndani ya 18 ambayo ilisababisha faulo baada ya mguu wake kwenda kwenye kichwa cha nahodha wa Simba, Method Mwanjale.

 Alipotafutwa Ajibu kuzungumzia hilo, alisema: “Kwangu ninajisikia furaha kwanza timu yangu kupata sare hii ambayo ninaamini imewafurahisha mashabiki wa Yanga. “Tuliingia uwanjani kwa nia moja ya kushinda ili tupate pointi tatu na tukae kileleni, lakini mipango ilikataa tukapata pointi moja,” alisema Ajibu.

No comments

Powered by Blogger.