Kidato cha Nne leo Jumatatu wameanza kutafanya mitihani ya Taifa
WATAHINIWA wapatao 385,938 wameanza kutafanya mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne leo Jumatatu, Oktoba 30, 2017 kote nchini. Akizungumza jana Jumapili, Oktoba 29,2017 Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde alisema kati ya watahiniwa hao, 323,513 (School candidates) ni wa shule na 62,425 ni wa kujitegemea (Private candidates).
Dk Msonde alisema mitihani hiyo
itaanza leo Oktoba 30, 2017 na kumalizika Novemba 17, 2017 huku akieleza
kuwa maandalizi ya mitihani yameshakamilika na mitihani imeshafika
kwenye vituo.
Aidha Msonde alizitaka kamati za
mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha utaratibu wa uendeshaji wa
mitihani hiyo unafuatwa huku akiwataka wanafunzi kuacha vitendo vya
udanganyifu wakati wa kufanya mitihani kwa kuwa wanaweza kufaulu bila
kufanya hivyo.
“Mliyojifunza yanatosha fanyeni
mitihani kwa kufuata utaratibu uliowekwa, baraza halitasita kuwafutia
mitihani wote watakaojihusisha na udanganyifu, wasimamizi wa mitihani
wajiepushe na vitendo vya udanganyifu, atakayekiuka atachukuliwa hatua
za kisheria.” alisema Msonde.

Post a Comment