ad

ad

Sababu zinazoweza kusababisha mimba kuharibika

KUNA wasomaji wengi wanapenda kujua sababu zinazoweza kusababisha mama mjamzito mimba yake kuharibika. Leo nitaelezea kwa kirefu ili wewe msomaji uweze kujua.


 Sababu kuu huwa ni magonjwa kama vile ugonjwa hatari wa malaria, ugonjwa unaotokana na zinaa kama vile kaswende, kisonono na U.T.I, dawa fulanifulani mfano albendazole, misoprostol, metronidazole na kadhalika. Lakini pia mjamzito akifanya kazi za kutumia nguvu nyingi anaweza kusababisha mimba yake kuharibika. 

Lakini kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha mimba
kutoka ambazo zinaweza kuzuilika kwa kwenda kliniki mapema, yaani pale tu unapohisi una mimba hata kama ni wiki mbili na kufuata ushauri wa wataalam. Ukweli ni kwamba, kuna wanawake wengi mimba zao huharibika na wao hushindwa kugundua mapema. 


DALILI ZA MIMBA KUHARIBIKA 
Zipo dalili ambazo husababisha mimba kuharibika kama tutakavyoona leo hapa; 

KUTOKWA DAMU NYINGI SEHEMU ZA SIRI 
Mjamzito akitokwa na damu nyingi sehemu za siri ni dalili
kwamba mimba imeanza kuachia na mlango wa uzazi umeanza kufunguka na hiyo inaashiria kwamba kuna mambo mawili yameshatokea. Kwanza inawezekana mtoto ameshafi a tumboni au bado hajafa, lakini kama damu imetoka kwa wingi,
inaashiria kuwa mtoto huyo aliye tumboni atakufa tu. 


MTOTO KUACHA KUCHEZA
 Ikiwa mtoto ataacha kucheza tumboni ni tatizo kubwa kwani kwa kawaida mtoto huanza kucheza akiwa wiki ya 18 mpaka 20 kwa wanawake ambao hawajawahi kubeba mimba na wiki ya 16 mpaka 20 kwa wanawake ambao wameshawahi kuzaa. Ikitokea mtoto aliye tumboni ameshawahi kucheza, lakini ghafl a akawa hachezi au muda huo umepitiliza na bado kimya, kuna uwezekano mkubwa ikawa
mtoto huyo amefi a tumboni, hivyo haraka sana wahi hospitali kumuona daktari. 


KUPOTEA KWA DALILI ZA UJAUZITO 
Kupotea kwa dalili za ujauzito ni tatizo lingine baya kwa mama mjamzito. Mara kwa mara mwanamke akiwa na ujauzito anakuwa na dalili nyingi kama vile kuwa na kichefuchefu, kukosa hamu ya kula baadhi ya vyakula, kutapika, kulamba vitu vichachu kama vile limao, ndimu, wengine hula udogo na wengi hubadilika sana tabia, hivyo basi dalili zote hizo za mimba zikisimama ghafl a, basi ujue mimba imeharibika. Itaendelea wiki ijayo

No comments

Powered by Blogger.