Rais Magufuli: Makonda Kwangu Ni Msomi Mzuri
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa hakuja kuuza sura bali kufanya kazi na kwamba mke wake akimpenda inatosha kwake.
Rais
Magufuli amesema hayo jana alipokuwa akihutubia Mkutano Mkuu wa 33 wa
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na kudai kuwa mkutano huo ni
muhimu sana kwake kwakuwa Serikali za Mitaa ziko karibu zaidi na
wananchi.
Alisema
watu wengi waliokuwa wananufaika na rasilimali za nchi hawawezi
kumpenda hata kidogo kwa mambo anayoyafanya lakini mke wake anatosha
kabisa kumpenda kwani hakuja kuuza sura.
Akitolea
mfano wa rasilimali za nchi, Rais Magufuli alisema hakuna nchi ambayo
mnaweza kuona rasilimali zenu zinachukuliwa halafu mnaacha na
kushangilia.
Alisema ndio maana kwenye Tanzanite wameamua kujenga uzio utakaogharimu sio zaidi ya shilingi bilioni sita (6).
Ndani
ya siku chache tu baada ya ujenzi wa ukuta kuanza, uzalishaji wa
Tanzanite umeongezeka takriban mara 30 zaidi na kwamba kuna siku
itapatikana zaidi ya kilo 18 za Tanzanite, kiwango ambacho hakijawahi
kutokea hapo awali.
Alisema katika mikataba ya madini, unakuta kabisa imeandikwa ‘hawa watu wasilipe ushuru’ na ni Mtanzania ametia saini.
“Mimi
ndiye Rais na ninajua siri zote za nchi hii, ni kuguswa tu na Roho
Mtakatifu hadi kushindwa kuwataja, na nikizungumza hivi waliokuwa
wananufaika hawawezi kunipenda,” alisema.
Aidha,
amemsifu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa mambo makubwa
anayofanya ikiwemo vita dhidi ya madawa ya kulevya.
“RC
Dar alipojaaribu kupambana na vita ya madawa ya kulevya ikawa kubwa
kwake, na wanasema hajasoma, mimi hata kama hajui A lakini anakamata
madawa ya kulevya, kwangu ni msomi mzuri,” amesema.
Rais
Magufuli alimuagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwaambia wakuu
wengine wa mikoa kuiga mfano wa Makonda ambaye anasikia ameweza
kukusanya Milioni 186.
“Nasikia
Mhe. Makonda umekusanya Milioni 186 na ninamuona anavyohangaika, Waziri
Mkuu kwanini viongozi wengine hawawezi kuiga kwa mwenzao?” amehoji Rais Magufuli.
Aliwapongeza
ALAT kwa kuamua kuhamia Dodoma ambapo Waziri Mkuu ameshahamia na Makamu
wa Rais amebakiza miezi 2 tu kuhamia, na yeye pia atahamia huko mwakani
na kuonya kuwa sasa aje amuone mtu atakayebakia Dar es Salaam.
Post a Comment