Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Askari wake Aliyefariki Dunia Kwa Kujipiga Risasi

Jeshi
la Polisi mkoani Pwani limezungumzia kifo cha askari wake PC Armand
Furaha (33) aliyejipiga risasi kifuani bila kukusudia na kufariki dunia.
Askari huyo alijipiga risasi hiyo usiku akiwa anaelekea kwenye lindo nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.
Tulio
hilo lilitokea saa moja usiku eneo la Mailimoja sokoni usiku wa kuamkia
jana, wakati askari huyo akiwa njiani kuelekea kwenye kituo cha lindo
alichopangiwa.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Pwani, Blasius Chatanda amesema askari huyo alijipiga
risasi bahati mbaya kwa bunduki aina ya SMG akiwa amekaa kwenye kiti
cha mbele katika gari alilokuwa anasafiria kwenda lindoni.
Amesema
uchunguzi wa awali umebaini kuwa askari huyo alikuwa tayari ameweka
risasi chemba kwenye bunduki hiyo aliyokuwa nayo na kwa bahati mbaya
akiwa anashuka kwenye hilo gari ndipo risasi hiyo ikafyatuka na kumpiga
kifuani eneo la kushoto na kufa wakati akipatiwa matibabu katika
Hospitali ya Tumbi.
“Kabla
ya tukio hilo, askari huyu aliwasili kazini jioni na kukuta amepangiwa
kituo cha ulinzi kwa mkuu wa wilaya hivyo kama ilivyo ada alichukua zana
za kazi ikiwemo bunduki hiyo na kuanza safari ya kuelekea lindoni kwake
huko kwa DC, lakini bahati mbaya hakufika alifariki kwa kujipiga risasi
bahati mbaya,” amesema Chatanda.
Akizungumzia
suala la askari kujipiga risasi Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera
Bulimba amesema kila tukio hutokana na mazingira tofauti.
Post a Comment