Nassari: Maisha Yangu Yapo Hatarini
Mbunge
wa jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari amefunguka na
kusema maisha yake yapo hatarini na kudai kuwa watu ambao amewaanika
kwenye sakata la ununuzi wa madiwani wanamtafuta.
Nassari
amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka alipokwenda kwa Mkurugenzi wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupeleka ushahidi
wake juu ya madiwani wa CHADEMA waliohama chama kwa kuhongwa rushwa na
wateule wa Rais John Pombe Magufuli.
"Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo hatarini kwani Watesi wetu wananitafuta" aliandika Nassari kupitia ukurasa wake wa facebook
Mbali
na hilo wachangiaji mbalimbali kwenye ukurasa wa Mbunge huyo walimtaka
azidi kumuomba Mungu huku wakimshauri kuongeza ulinzi zaidi katika
maisha yake ya kila siku kutokana na jambo ambalo ameliibua na kumtaka
aendelee kupambana, baadhi ya wachangiaji wengine wamedai kuwa
anachofanya ni njia ya kujitafutia umaarufu kisiasa.
Juzi
Mbunge Joshua Nassari, Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini
Mchungaji Peter Msigwa walikwenda kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) na kupeleka ushahidi wao juu ya sakata la
kununuliwa kwa madiwani wa CHADEMA na kuhongwa fedha na ahadi mbalimbali
kutoka kwa wateule wa Rais mkoani Arusha.
Post a Comment