Picha za kwanza ya Tundu Lissu akiwa hospitalini Nairobi
Mbunge wa Singida Magharibi, Tundu Lissu akipunga mkono.
Baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe jana kuahidi mbele ya waandishi wa habari kwamba picha za Mbunge wa Singida Magharibi, Tundu Lissu, zingeanza kutoka kuonyesha afya yake ilivyoimarika hospitalini Nairobi ambako alipelekwa baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana huko nyumbani kwake Dodoma, leo chama hicho kimetokea picha ya kwanza.
Akiwa kwenye wheel chair.
Madhumuni ya kutoa picha hizo, kwa mujibu wa Chadema, ni kuwahamasisha Watanzania waendelee kumchangia fedha na kumuombea afya yake iimarike ikiwa ni pamoja na kuwatia moyo wale ambao walimchangia mwanzoni kabisa alipopatwa na mkasa huo.
Kwa mujibu wa chama hicho, Lissu sasa anatembea kwa kutumia kiti maalum cha magurudumu (wheel chair), anaongea na kula chakula anachokitaka.
Vilevile, muda wowote tangu sasa, chama hicho kimesema kitatoa video kumwonyesha Lissu akiongea.

Post a Comment