Baada ya Kuona Hali ya Tundu Lissu, Sheikh Ponda Azungumza Haya
Sheikh Issa Ponda.
“Tulipokuwa tunabadilisha mawazo, niliguswa na hisia kubwa, badala ya mimi kumpa matumaini yeye ndiye alinipa matumaini,” amesema Ponda.
Amesema madhumuni ya safari yake yalikuwa kumjulia hali Lissu, kumwombea dua, kumjengea matumaini ya afya na kujenga mazingira mapana yanayotosha kulizungumza jambo lililomfika.
Lissu anapata matibabu katika Hospitali ya Nairobi baada ya kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 akiwa nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Sheikh Ponda amesema Lissu alimweleza hivi karibuni atarudi katika harakati na ataanzia alipoishia.
“Amehimiza mshikamano na alionyesha ana matumaini na Watanzania kwa harakati wanazozifanya,” amesema.
Aidha Polisi walifika eneo hilo kwa lengo kuzuia mkutano huo usifanyike lakini walikuwa wamechelewa kwani Sheik Ponda alikuwa ameshamaliza kuzungumza na wanahabari, hivyo askari hao waliwakamata baadhi ya wanahabari ambao hata hivyo baadaye waliwaachia.
Post a Comment