Mtoto Aelezea Alivyomkuta Mkuu Wa Shule Amejinyonga
Frank Benedicto (14) ni mtoto mkubwa wa Mkuu wa
Sekondari ya Migukulama, Benedicto Lweikiza (45) aliyejinyonga juzi,
amesema alitahamaki kumkuta baba yake akiwa amening’inia darini.
Lweikiza
alijinyonga hadi kufariki juzi saa tisa alasiri katika mtaa wa Kilabela
Kata ya Nyatukala wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
Mwalimu huyo alikuwa anafundisha Sekondari ya Migukulama iliyopo Kata ya Nyanzenda Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema.
Mtoto
wa marehemu huyo aliyekuwa akiishi na baba yake kwenye nyumba hiyo,
anasoma kidato cha kwanza katika Sekondari ya Sima iliyopo wilayani
hapo, alisema baada ya kutoka shuleni alikuta mlango wa nyumba yao upo
wazi hivyo akadhani baba yake atakuwa kwa majirani.
NE
NE
“Asubuhi
niliagana vizuri na baba yangu wakati nikienda shuleni, jioni
niliporudi ndipo nikakuta baba amejinyonga juu ya dari na kabla
sijagundua kitu chochote nilikuta mlango wa nyumba upo wazi nikadhani
yupo kwa majirani nilipoingia chumbani sikuamini nilichokiona mbele
yangu,” alisema
Alisema baada ya kuona hivyo alitahamaki na kuanza kupiga kelele ndipo majirani walifika kushuhudia tukio hilo.
Mmoja
wa majirani hao, Silvesta Juma alisema kabla marehemu hajajinyonga
walikuwa wote asubuhi wakibadilishana mawazo na wakaachana salama hivyo
alishtuka kukuta amejinyonga.
Martha Mabula ni
mwanafunzi wa kidato cha pili shule aliyokuwa akifundisha mwalimu huyo,
alisema “Kifo cha mwalimu wetu kimeshtua wengi na kuacha simanzi kubwa
na pengo hili litachukua muda kuliziba.”
Msemanji wa
familia hiyo, Martin Kalemera alisema kuwa maiti atasafirishwa kutoka
Hospitali ya Wilaya ya Sengerema ilipokuwa imehifadhiwa na kwenda
kuzikwa leo kijijini kwao Kasisa Buchosa.
Alisema hadi
sasa hakuna taarifa rasmi zilizopatikana za ndugu yao kujinyonga kwa
sababu hakuacha ujumbe wowote wala familia haikuwa na taarifa zozote
mbaya dhidi ya ndugu yao.
Alisema marehemu ameacha
watoto watatu. Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole alisema kuwa
vyombo vya Dola vinafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo na kusema kuwa
watatoa taarifa baadaye baada ya uchunguzi kukamilika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema jeshi la polisi linaendela kufanya uchunguzi wa kifo hicho.
By Daniel Makaka, Mwananchi
By Daniel Makaka, Mwananchi
Post a Comment