WAZIRI MWIJAGE AFUNGUA KIWANDA CHA MABATI CHA ALAF MKOANI DODOMA
Mgeni
rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Kiwanda cha kutengeneza mabati cha
Kampuni ya ALAF Kanda ya Dodoma, Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Charles Mwijage (mwenye tai), Waheshimiwa Wabunge ambao ni
Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Viwanda pamoja na Viongozi
wajuu wa Kampuni ya ALAF Tanzania wakishirikiana kukata utepe pamoja na
kuashilia ufunguzi wa kiwanda cha mabati cha ALAF kanda ya kati mjini
Dodoma.
Kampuni
ya ALAF (Tanzania) imefungua tawi lake jipya Mkoani Dodoma ikiwa ni
kutekeleza maagizo ya Sera ya Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma kwa
wananchi baada ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza,
Mbeya na Arusha.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Charles Mwijage alisema "Napenda kuwahakikishia kwamba Serikali yetu
inafanya kila linalowezekana
kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa sehemu muhimu ya kuwekeza kwa
kulinda mitaji yao kupitia kuondoa ushindani usiokuwa wa haki hasa
unaotokana
na baadhi ya wafanya biashara kudanganya thamani ya bidhaa za bati
zinazoingizwa toka nje ya nchi na kulipa kodi pungufu, kudhibiti
uingizaji
wa bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora na zaidi kulinda amani na
maelewano
yaliyopo baina ya Serikali na wadau mbalimbali ili kujenga ustawi wa
nchi yetu.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akifungua jiwe la
msingi la kiwanda cha mabati cha ALAF Dodoma kwa ajili ya kuhudumia
wananchi wa mikoa ya kanda ya kati (Dodoma, Singida na Tabora), Kushoto
ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty.
Waziri Mwijage aliendelea kwa kusema “Napenda kuwashukuru
Kampuni ya ALAF (Tanzania) Ltd kwa kutekeleza vizuri maelekezo ya Sera ya
Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma zao kwa wananchi wa Dodoma baada
ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.”
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty alisema "uwekezaji
huu wa Dodoma ni wa thamani ya shilingi bilioni tatu ukiajiri watu 15 moja kwa moja
na wengine zaidi ya 100 ajira zisizo za moja kwa moja kama kupakia na
kushusha bati, kusafilisha bati, huduma za maji, stationary n.k."
Pia aliongeza kwa
kusema "ALAF inakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo uagizaji wa
bidhaa sizizokidhi viwango unaofanywa na makampuni mbalimbali na pia
ukwepaji wa kodi, kupelekea serikali kukosa mapato stahiki na walaji kutumia
bidhaa zilizo chini ya viwango na hii hupelekea kukatisha tama wawekezaji wa
ndani ambao wanajitaidi kuzalisha bidhaa zenye ubora na kulipa kodi zote
stahiki.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) akimueleza
jambo Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty.
ALAF
imekuwa ikishiliki
kwenye kama vile elimu, makazi, afya na mazingira.Mpaka sasa ALAF
imetumia takriban shilingi milioni 200 kwenye mradi wa kuwaelimisha
wafanyakazi na jamii kuhusu
ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa kushilikia na shirika la fedha
duniani.
Alikadhalika kwa upande wake Meneja wa ALAF kanda ya kati, Grayson
Francis Mwakasege nae aliongeza kwa kusema ufunguaji wa kiwanda hiki
Dodoma umeleta ahuenei kwa wakazi wa kanda ya kati Dodoma, Singida na
Tabora ambao hapo mwanzo walikuwa wakiagiza bati kutoka Dar es salaam kwa ghalama ya
kati ya sh 3000 - 5000 kwa bati la rangi lenye urefu wa kuanzia mita 3 na
kuendelea. Pia aliongelea uwezo wa machine zilizofungwa Dodoma kuwa zinaweza kuzalisha tani 50 sawa na nyumba 50 kwa siku.
Uzinduzi huo pia ulihudhuliwa na kamati ya bunge ya uwekezaji na viwanda pia
wabunge kutoka Dodoma na Singida pamoja na mkuu wa wilaya ya Chamwino pia
wakurugenzi wa wilaya za Dodoma.
Wageni waalikwa toka mikoa ya kanda ya kati Dodoma, Singida na Tabora.
Meneja
wa ALAF kanda ya kati, Grayson Francis Mwakasege akizungumza jambo
katika hadhira iliyofika kwa ajiri ya uzinduzi wa kiwanda cha
mabati cha ALAF tawi la Dodoma kwa ajiri ya kuhudumia mikoa ya kanda ya
kati.
Picha ya pamoja kati ya mgeni rasmi na wafanyakazi wa ALAF ,wakurugenzi wa wialya za Dodoma
pamoja na wabunge wa mkoa wa Dodoma na Singida
Post a Comment