Tundu Lissu Apigwa Risasi, Akimbizwa Hospitali
MBUNGE wa Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumpiga risasi zinazodaiwa kuwa tano.
Tukio hilo linadaiwa kutokea leo akiwa nyumbani kwake Dodoma ambapo watu hao walimvamia akiwa kwenye gari kisha kumpiga risasi.
“Ni kweli, Tundu Lissu amepigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake, amekimbizwa katika Hospitali ya Mkoa, Dodoma. Na mimi nipo njiani naelekea huko hospitali kumuona,” alisema Mbowe.
Taarifa zaidi endelea kufuatilia mitandao yetu.

Post a Comment